Marioo Kufanyia Uzinduzi Video Yake Ya ‘Dear X’ Hivi Karibuni

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Marioo ameendelea kutikisa kiwanda cha muziki Tanzania baada ya kutangaza kufanya uzinduzi mkubwa wa video ya wimbo wa Dear Ex ambayo inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Marioo aliachia ngoma ya "Dear Ex" Juni 22 mwak 2022 ikiwa ni mara nyingine tena kwa msanii huyo kuachia ngoma ya Amapiano ambapo tangu kuachiwa kwake Dear Ex imekuwa ni ngoma pendwa baina ya mashabiki wa muziki nchini Tanzania kutokana na mashahiri yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marioo ambaye anatarajiwa kuachia albamu yake ya kuitwa "The Boy You Know" hivi karibuni ametangaza kuwa anatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa video ya "Dear Ex" siku Septemba 11 ambapo uzinduzi huo utafanyika Kidimbwi Beach Jijini Dar Es Salaam.

Mashabiki kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiisubiri video hiyo kutoka kwa Marioo. Video ya Dear ya Ex kutoka  kwa Marioo inatarajiwa kuwa video ya tatu kutoka kwa Marioo kwa mwaka 2021 baada ya kuachia Te Amo mwezi Februari pamoja na Naogopa video ambayo aliitoa mwezi mwaka huu akiwa na Harmonize.

Kando na Marioo, msanii mwingine kutoka Tanzania ambaye ameshawahi kufanya uzinduzi wa video ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye mapema mwaka huu alizindua video za muziki 10 kutoka kwenye EP yake ya First Of All pale Cinemax Century, Mlimani City, Dar Es Salaam.

Leave your comment