Chelsea Yamfuta Kibarua Thomas Tuchel

[Picha: mirror.co.uk]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya umiliki mpya wa chelsea ukiwa chini ya Todd Boehly kuanza kazi kwa takribani siku 100 na zaidi zilizopita, sasa uongozi huo umeamua kumfuta kazi kocha Thomas Tuchel mapema Jumatano ya tarehe 7 ya mwezi wa tisa.

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii kama vile Twitter pamoja na Instagram klabu hiyo ya soka imeandika waraka ukielezea kumfuta kazi kocha huyo pamoja na benchi lake la ufundi. Kufukuzwa huko kwa kocha huyo ni kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata katika ligi kuu ya Uingereza pamoja na kuanza mechi ya mabingwa Ulaya kwa kufungwa bao moja na Dinamo Zagreb.

Uongozi huo mpya wa Chelsea umekwazika na kiwango cha uchezaji cha timu hiyo licha ya Thomas kupatiwa kitita cha pesa na kufanya usajiili kwa wachezaji aliowahitaji katika msimu huu.Wachezaji aliowasajili kwa msimu huu ni kama vile Raheem Sterling kutokea Manchester city, Pierre Emerick Aubameyang alitokea Barcelona pamoja na wachezaji wengine

Akiwa na Chelsea tayari kocha huyo ameweza kuifanikisha Chelsea kuchukua ubingwa wa mabingwa Ulaya yaani Champions League, klabu bora ya dunia kwa maana ya Club world Cup,  pamoja na Super Cup tangu January 2021 alipojiunga huko Stanford Bridge.

Baada ya tamko hili klabu hiyo imesema wachezaji wake wataendelea kupewa mafunzo na wafanyakazi waliobaki mpaka pale kocha mpya atakapo patikana. Hii itasaidia wachezaji waweze kujiandaa na mashindano mengine yanayofuatia.

Bila ya hiyana klabu hiyo ya soka imetoa shukrani zake kwa kocha huyo katika mafanikio yake yote waliyoyapata na kuongeza kuwa Tuchel atakuwa moja ya walioweka historia katika klabu hiyo baada ya kushinda mashindano mbalimbali akiwa na Chelsea.

Ikiwa bado Chelsea inatafuta Kocha mpya baadhi ya makocha wameweza kuhusishwa na fununu za kuwasili klabuni hapo . Baadhi ya makocha hao ni akiwemo Zindine Zidane, Mauricio Pochettino  pamoja na Potter Rodgers

Leave your comment