Collabo Tano Bora Za Kimataifa Za Diamond Platinumz

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ni suala lililo wazi kuwa msanii Diamond Platnumz ndiye msanii anayeiwakilisha muziki wa Bongo Fleva kimataifa ambapo kupitia nyimbo zake Diamond ameweza kupenya na kujulikana katika mataifa mbalimbali ikiwemo Nigeria, Kenya, Ghana, Uganda na mataifa mengine mengi.

Kushinda tuzo kama MTV EMA za Ulaya, Headies za nchini Nigeria, Afrimma na nyinginezo nyingi ni ushahidi tosha kuwa Diamond Platnumz ni msanii wa kimataifa na moja kati ya vitu ambavyo vimepelekea Diamond Platnumz kujulikana kimataifa ni collabo zake ambapo msanii huyo amekuwa akishirikiana na wasanii wa, mataifa mengine.

Zifuatazo ni collabo 5 kali za kimataifa  kutoka kwa Diamond Platnumz :

Yope Remix - Innos B

Hii ni ngoma ambayo Diamond Platnumz alishirikiana na msanii Innos B kutokea nchini Congo. Yope Remix iliweza kuitambulisha vyema Bongo Fleva nchini Congo kiasi cha kuwa video ya muziki kutoka Tanzania ambayo imetazamwa zaidi Youtube kwani kufikia sasa imetazamwa mara Milioni 194 kwenye mtandao huo

https://www.youtube.com/watch?v=ebZ7Ng1okCg

African Beauty - Marion.

Ngoma hii ambayo Diamond Platnumz alimshirikisha Marion kutokea nchini Marekani ilikuwa na lengo la kumtambulisha Diamond Platnumz huko ughaibuni hasa Amerika ya Kaskazini. Wimbo huu ulipokelewa vyema sana kwani kiasi cha kushinda kipengele cha collaboration bora ya mwaka kwenye tuzo za AEUSA mwaka 2018.

https://www.youtube.com/watch?v=KjNl1FXE0A8

Nana - Mr Flavour.

Nana ni moja kati ya collano bora kuwahi kutokea baina ya msanii wa Tanzania na mwanamuziki wa Nigeria. Ukiweka kando ubora wa ngoma ya "Nana", video ya ngoma hii ambayo iliyoongozwa na Godfather Productions ilichagiza wasanii wengi sana watanzania kwenye kuandaa video zao za muziki huko nchini Afrika Kusini.

https://www.youtube.com/watch?v=IflpfcHmq5I

My Number One Remix - Davido

Hii ni ngoma ambayo ilimtambulisha Diamond Platnumz na Bongo Fleva kwa ujumla kwenye medani za muziki wa Afrika. Kupitia ngoma hii, Diamond Platnumz alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa la kubwa la tuzo za  MTV MAMA huko Afrika ya Kusini na pia alishinda tuzo mbalimbali kama Chanel O, tuzo za Hipipo na nyinginezo nyingi.

https://www.youtube.com/watch?v=Cd2bwLcgGGg

Hallelujah - Morgan Heritage.

Kwenye ngoma hii, Diamond Platnumz alishirikiana na kundi la Morgan Heritage. Namna ambavyo Bongo Fleva iliweza kujichanganya vyema na muziki wa Reggae kwenye ngoma hii ni kitu cha kupigiwa makofi. Ngoma hii iliweka rekodi mpya baada ya kufikisha watazamaji Milioni 1 ndani ya saa 15 tu na watazamaji Milioni 2 ndani ya siku mbili tu.

https://www.youtube.com/watch?v=JPJ3_aR9l0I

Leave your comment