Mabantu Waachia Ngoma Mpya "Leo" Wakimshirikisha Marioo

[Picha: Screengrab/Youtube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kundi la muziki linalofanya vizuri sana nchini Tanzania kwa sasa, Mabantu limeachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa "Leo" ambayo wamemshirikisha mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa Marioo.

Ngoma hii mpya ya Mabantu ya kuitwa "Leo" inakuja takriban miezi minne tangu kundi hilo linaloundwa na Twaha pamoja na Muh Mabantu kuachia ngoma yao ya kuitwa "Star" ambayo baada ya kufanya vizuri kwa ngoma hiyo nchini Tanzania, Rayvanny aliungana na Mabantu kisha kuachia "Utamu Remix".

Leo ni ngoma ambayo Mabantu wanatumia vipaji vyao kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa sehemu yao waliyofikia leo ambapo wanatoa shukrani kwa mambo tofauti, huku Marioo nae akisikika zaidi kwenye ubeti wa pili ambapo nae anatumia mashahiri mazuri kushukuru kwa kumpata mwenza wake na kuweza kuwanyamazisha wasiompenda.

Ngoma hii imetayarishwa na Gachi B, ambaye pia alishiriki kuandaa ngoma ya Utamu ya Mabantu na kufikia sasa ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kutoka Tanzania ikiwemo CEO wa Next Level Music  Rayvanny pamoja na Rais wa Konde Gang, Harmonize ambaye hivi karibuni ametangaza kuachia ngoma mbili.

https://www.youtube.com/watch?v=IPdEwqR1ECg

Leave your comment