Uchambuzi Mechi ya Manchester United Vs Arsenal
5 September 2022
[Picha: talksport]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Manchester United wameendelea kupaisha bendera yao kwa kunyakua alama tatu zingine mbele ya Arsenal. Mchezo huo uliochezwa huko Old Trafford umekuwa mchezo wa kwanza kwa Arsenal kufungwa katika msimu huu. United wamemaliza dakika 90 kwa kuwafunga Arsenal jumla ya magoli 3-1.
Goli la kwanza lilifungwa na mbrazili Antony ambaye ana siku mbili pekee tangu aanze mazoezi na United. Goli hilo alilolifunga winga huyu ni baada ya Marcus Rashford kumpatia pasi ya usaidizi wa goli katika dakika ya 35 ya mchezo.
Arsenal nao hawakubaki baki nyuma baada ya kipindi cha pili kuanza Bukayo saka naye akasawazisha bao hilo katika dakika ya 60 ya kipindi cha pili. Hilo limekuwa bao la kwanza kwa winga huyo wa kulia kutokea Arsenal kwa msimu huu.
Magoli mawili ya United yote yalifungwa na straika Marcus Rashford baada ya goli la pili kupokea pasi ya usaidizi wa goli kutoka kwa Bruno Fernandez katika dakika ya 66. Katika dakika ya 75 kiungo mshambuliaji Christiani Ericksen bila hiyana akatoa pasi ingine kwa Rashford na kukamilisha mabao 3-1 dhidi ya The Gunners.
Katika mechi hiyo Arsenal waliongoza kutawala mchezo kwa 60% na United wao walitawala mchezo huo kwa asilimia 40 pekee. Kwa upande wa kona United walikuwa na jumla ya 2 wakizidiwa na Arsenal ambao wao walikuwa na kona 5.
Katika upande wa maoteo United walipata maoteo 4 huku wao Arsenal wakiwwa hawana maoteo yoyote. Kadi za njano zilikuwepo kwa timu zote mbili kupata jumla ya kadi tatu huku kukiwa hakiina kadi nyekundu iliyotolewa.
Baada ya mchezo kuisha Arsenal wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 15 baada ya kupoteza mechi moja. Huku Manchester united wao wakiwa na alama 12 katika ushindi wa mechi 4 mfululizo.
Leave your comment