Collabo 5 Bora Za Kimataifa Kutoka Kwa Alikiba

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Toka aanze muziki miaka kadhaa iliyopita mwanamuziki Ali Kiba amekuwa ni mmoja ya wasanii wachache kutoka Tanzania ambaye amekuwa akiiwakilisha Bongo Fleva vyema katika medani za kimataifa kwa maana ya Afrika na nje ya Afrika. Sauti yake mujarab, mashahiri yake ya kuvutia na kubwa kabisa kupendelea kufanya collabo na wasanij wa nje ni baadhi ya vitu vilivyochagiza ukubwa wake katika muziki wa kimataifa.

Zifuatazo ni collabo 5 bora kutoka kwa Ali Kiba ambazo ameshirikiana na wasanii wa kimataifa:

Salute - Rudeboy

Ali Kiba aliachia collabo hii mwaka 2021 na bila shaka ngoma hii ambayo ilisindikizwa na video nzuri yenye hadhi ya kimataifa iliweza kumtambulisha vyema Ali Kiba nchini Nigeria.

https://www.youtube.com/watch?v=oQ8SycSejrM

Unconditionally Bae - Sauti Sol

Kwenye ngoma hii ambayo ameshirikishwa na Sauti Sol, Ali Kiba aliweza uwezo wake wa kucheza na sauti kwa kiwango cha juu sana. Ngoma hii iliweza kuimarisha hadhi ya Ali Kiba kama mfalme wa muziki huu wa Bongo Fleva kwa huko nchini Kenya, kwani wimbo huu uliweza kufanya vizuri Afrika Mashariki kwa ujumla.

https://www.youtube.com/watch?v=pLs4Tex0U1U

Aje Remix - MI

Ukiweka kando sauti nzuri ya Ali Kiba kwenye kibao hiki, pia mashahiri na michano makini ya rapa MI kutoka nchini Nigeria iliweza kufanya wimbo huu kuwa maarufu sana. Hii ni nyimbo ambayo ilichagiza Ali Kiba kushinda kipengele cha msanii bora Afrika mbele ya Wizkid mwaka 2016 kwenye tuzo za MTV EMA

https://www.youtube.com/watch?v=DtoRQXXjJSI

Niteke - Blaq Diamond

Ali Kiba aliweza kuchangamsha albamu yake ya "Only One King" kupitia collabo yake hii na kundi la Blaq Diamond kutokea Afrika Kusini. Ngoma hii ilipokelewa vyema na mashabiki hasa baada ya video yake ambayo imeja na ubunifu wa aina yake kuachiwa mapema mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=l696Po6vjwo

Happy - Sarkodie

Muingiliano mzuri wa sauti pamoja na utashi wa Ali Kibawa kuweza kubaki kwenye asili yake yaani Bongo Fleva. Pamoja n kwamba ngoma hii bado haina video lakini bila shaka iliweza kumtambulisha vyema Ali Kiba kiwanda cha muziki nchini Ghana.

https://www.youtube.com/watch?v=CjljpOF9LIU

Leave your comment