Diamond Platinumz Ashinda Tuzo Za Headies Nchini Nigeria

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki na CEO kutoka lebo ya WCB Wasafi Diamond Platnumz kwa mara nyingine ameweka historia mpya kwenye Bongo Fleva baada ya kushinda tuzo za Headies kutoka nchini Nigeria.

Kwa mwaka huu, Tuzo za Headies ambazo zilikuwa kwenye toleo lake la 15 tangu kuanzishwa kwake zilifanyika huko Atlanta nchini Marekani Jumapili ya Septemba 4 mwaka 2021 na kuhudhuriwa na mastaa wakubwa kutoka nchini Nigeria kama Patoranking, Adekunle Gold, Asake, Fire Boy DML, Olamide, D'Banj, BNXN na wengineo wengi.

Diamond Platnumz ameshinda kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki ambapo katika kipengele hicho alikuwa akichuana na wasanii wengine kama Harmonize na Zuchu kutoka Tanzania, Meddy kutokea Rwanda, Eddy Kenzo kutokea Uganda pamoja na Nikita Kering kutokea nchini Kenya.

Aidha Diamond Platnumz pia alitajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa Afrika, kipengele ambacho ameshinda msanii kutokea Nigeria wa kuitwa Burna Boy ambaye katika tuzo za mwaka huu ameshinda tuzo ya msanii bora wa Afrika pamoja na msanii bora wa kiume kutokea Nigeria.

Hii si mara ya kwanza kwa Diamond Platnumz kutajwa na tuzo za Headies kwani mwaka 2014 pamoja na mwaka 2015 Diamond Platnumz alitajwa kuwania kipengele cha Msanii Wa Afrika katika tuzo hizo za Headies lakini hakuweza kushinda.

Leave your comment