Wasanii Wa Singeli Ambao Wameshawania Na Kushinda Tuzo Mbalimbali Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Muziki wa singeli umeendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania ambapo wasanii wa muziki huo wamekuwa wakitumbuiza kwenye majukwaa makubwa Tanzania kama Fiesta pamoja na Mziki Mnene lakini pia wasanii hao wamekuwa wakishinda tuzo mbalimbali hasa za ndani ya nchi yaani Tanzania.

Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao wameshawahi kubeba Tuzo katika safari yao ya muziki :

Sholo Mwamba

Sholo Mwamba aliweza kutikisa Tanzania mapema mwaka huu baada ya kushinda tuzo 3 kwenye Tanzania Music Awards 2022 mojawapo ikiwa ni Msanii bora wa Singeli kwa mwaka huo akiwashinda wasanii wengine kama Dulla Makabila pamoja na Meja Kunta.

Snura Mushi

Kwenye tuzo za Tanzania Music Awards mwaka huu Snura alikuwa ni mwanamuziki wa kwanza wa kike wa Singeli kushinda tuzo kipengele cha Msanii Bora wa Kike Singeli mbele ya wasanii wengine kama Mimah, Rehema Hamis Tajiri pamoja na Lamona

Man Fongo

Baada ya kuachia "Hainaga Ushemeji" mwaka 2016 Man Fongo alipata umaarufu mkubwa kiasi cha kushinda tuzo ya msanii bora chipukizi kwenye tuzo za ambazo ziliandaliwa na kituo cha East Africa Television yaani EATV kwa mwaka huo.

Tuzo hii iliongeza kwa ukubwa umaarufu wa Man Fongo na kukudha hadhi yake kama Msanii.

Dulla Makabila

Kwenye tuzo za Tanzania Music Awards 2022, Dulla Makabila alitajwa kuwania kipengele cha mtumbuizaji bora wa kiume wa mwaka ambapo aliweza kuchuana na wasanii wengine wa Bongo Fleva kama Ali Kiba pamoja na Harmonize.

Leave your comment