Nyimbo Mpya: Billnass 'Utaonaje' , Rich Mavoko 'Fanya Urudi' na Nyimbo Nyingine Mpya wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ikiwa ni Wiki ya mwisho kabisa ya mwezi Agosti, wasanii wengi kutokea Tanzania wameendelea kuachia ngoma mpya ambazo zimeendelea kuchangamsha kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva.

Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka Tanzania Wiki Hii:

Napendwa II - Mocco Genius Ft Ali Kiba.

Baada ya toleo la kwanza kufanya vizuri, mtayarishaji wa muziki ambaye kwa sasa amehamia kuwa mwanamuziki, Mocco Genius ameachia "Napendwa II", akiwa na Ali Kiba. Sauti nzuri ya Ali Kiba pamoja na mashairi mazuri kutoka kwa Mocco Genius yamefanya ngoma hii kuwa ya kipekee sana.

https://www.youtube.com/watch?v=MIqMJVxZ-KA

Utaonaje - Billnass Ft Rayvanny

Rayvanny na Billnass wameungana kwa pamoja kwenye "Utaonaje", ngoma ambayo ndani yake wasanii hawa wanajisifia kwa kuishi vizuri huku wakisema wabaya wao kwa maneno ya kukera na ya kuudhi.

https://www.youtube.com/watch?v=L_3o4-4UK7I

Hadithi (Video) - Barnaba Classic Ft Diamond Platnumz

Hatimaye mwanamuziki Barnaba Classic ameachia video ya ngoma yake ya "Hadithi" akimshirikisha Diamond Platnumz. Video hii imefanyika nchini Afrika Kusini ikiongozwa na Justin Campos huku baadhi ya vipande vikiwa vimeongozwa na Hanscana kutoka Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=-JaiCotheaU

Fanya Urudi - Rich Mavoko Ft Gemini Major

Rich Mavoko ameendelea kuthibitisha kuwa yeye ni fundi wa Bongo Fleva baada ya kuachia "Fanya Urudi", ngoma ambsyo ukiweka mashairi yake mepesi lakini mitindo mizuri ya dansi pamoja ubora wa picha umeweza kupamba video hii ambayo kufikia sasa imeshakusanya takriban watazamaji laki moja thelathini huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=ui6bhU46hqY

Haula - Nedy Music Ft Dayo.

Haula ni ngoma ya wapendanao ambayo ndani yake Nedy Music anaeleza sifa alizonazo mpenzi wake pamoja na kuonesha ni kwa namna amezama kwa mwemza wake.

https://www.youtube.com/watch?v=b5efL6yfssY

Leave your comment