Mbosso Atangaza Kuachia Ep Yake Hivi Karibuni

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki kutokea lebo ya WCB Wasafi Mbosso kwa mara nyingine ametetemesha kiwanda cha muziki Tanzania baada ya kutangaza ujio wa EP yake mpya hivi karibuni.

Mbosso ambaye hivi karibuni aliachia ngoma yake ya kuitwa "Moyo" akiwa na Costa Titch kutoka Afrika Kusini alitoa taarifa hizo hivi karibuni ambapo amesema kuwa muda wowote kutokea sasa ataachia EP yake ambayo bado hajatangaza jina lake.

Mbosso ametoa taarifa hiyo hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Bingwa wa Mtaa ya Wasafi Bet.

"Tunaandaa vitu vingine, Mungu akijaalia, muda wote kutokea sasa hivi nitatoa EP yangu" alizungumza Mbosso.

Kufikia sasa Mbosso ameachia albamu moja ya kuitwa "Definition Of Love" ambayo imetoka mwezi Machi mwaka 2021 ambapo Mbosso alishirikisha wasanii tofauti tofauti ikiwemo Diamond Platnumz, Baba Levo na Liyaah kutokea nchini Nigeria a albamu hiyo ilitajwa moja kati ya albamu zilizofanya vizuri kwa mwaka huo wa 2021.

Kando na Mbosso wasanii wengine kutoka WCB ambao wameshaachia EP zao ni pamoja na Lavalava ambaye aliachia "Promise EP", Zuchu ambaye mwezi Aprili mwaka 2020 aliachia EP yake ya kuitwa "I Am Zuchu" pamoja na Diamond Platnumz ambaye alitikisa mwaka huu baada ya kuachia "First Of All" EP mapema mwaka huu.

Leave your comment