Nyimbo Mpya: Barnaba Classic 'Hadithi', Nandy 'Napona' na Nyimbo Zingine Zinazovuma Tanzania Wiki Hii
26 August 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo
Bila shaka kama unafuatilia muziki kutoka nchini Tanzania, kufikia sasa utafahamu kuwa wiki hii kuna baadhi ya nyimbo ambazo zimeweza kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube kutokana na mashabiki kupendelea kutazama au kusikiliza ngoma hizo kwenye mtandao huo.
Zifuatazo ni ngoma tano kutoka nchini Tanzania ambazo zinafanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube :
Hadithi - Barnaba Classic Ft Diamond Platnumz
Ngoma namba 1 kwenye albamu ya, Barnaba Classic ya kuitwa "Love Sounds Different" imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube. Mashahiri mazuri pamoja na ushirikiano wa aina yake umesababisha ngoma hii kupendwa sana na mashabiki.
Marry Me - Barnaba Classic Ft Marioo
Hii ni moja kati ya ngoma bora kwenye albamu ya Barnaba Classic hasa ukizingatia sauti nzuri ya Marioo ambayo inafungua ngoma hii pamoja na mashahiri mujarab ya Barnaba ambayo yanapamba sehemu ya pili ya ngoma hii.
Napona - Nandy Ft Oxlade
Wiki mbili tangu kuachiwa kwake, video ya Napona ya kwake Nandy akiwa na Oxlade imeendelea kufanya vizuri. Ukiweka kando video hii kuwa na stori nzuri lakini pia ubora wa picha pamoja na mitindo bora kabisa ya dansi imeweza kufanya video hii kuwa ya kipekee sana.
Fire - Zuchu
Zuchu ameendelea kukoleza umalkia wake kwenye muziki wa Tanzania kupitia video yake ya hivi karibuni ya kuitwa "Fire" ambayo imepokelewa kwa mikono miwili na mashabiki nchini na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 3.7 kwenye mtandao wa YouTube.
Yanga - Marioo
Mashabiki wa timu ya Yanga wameendelea kumuunga mkono Marioo kupitia ngoma yake ya hivi karibuni ya kuitwa "Yanga" ambayo sio tu kwamba imeweza kuburudisha mashabiki wa Yanga pekee lakini kila mtu atakayesikiliza ngoma hii ataweza kukubali kipaji cha uandishi wa Marioo.
Leave your comment