Hatimaye Barnaba Classic Aachia Albamu Yake "Love Sounds Different"

[Picha: Barnaba Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kutokea nchini Tanzania Barnaba Classic kwa mara nyingine ameweza, kutikisa kiwanda cha Bongo Fleva baada ya kuachia albamu yake mpya kabisa ya kuitwa "Love Sounds Different".

Barnaba Classic amekuwa akidokeza kuhusu ujio wa albamu kwa muda mrefu sasa kupitia mahojiano na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambapo usiku wa kuamkia aliweza kufanta uzinduzi wa albamu hiyo kwenye ukumbi wa Mlimani City Hall Dar Es Salaam, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na wasanii mbalimbali kama Diamond Platnumz, Marioo, Mbosso, Zuchu na wengine wengi.

Soma pia: Cheed Aachia Tracklist Ya Ep Yake Ya "Endless Love"

Albamu ya "Love Sounds Different" imesheheni ngoma 19 ambapo kati ya hizo ngoma zote ameweza kushirikisha wasanii tofauti tofauti wakali kutoka Afrika Mashariki kama Diamond Platnumz, Jux, Rayvanny, Alikiba, Nandy, Marioo, Young Lunya, Khaligraph Jones, Jay Melody, Lady Jaydee, Platform TZ, Lody Music Saraphina, Dayoo, Khadija Kopa, Kusah, Joel Lwaga.

Aidha mwanamuziki Diamond Platnumz ameweza kushiriki Mtayarishaji Mkuu wa albamu hiyo (Executive Producer) huku watayarishaji wengins waliohusika katika albamu hiyo ni pamoja na Lizer Classic, Abbah Process, S2kizzy, Mr. Simon, Chizan Brain pamoja na Wanene Studios.

Kando na kuachia albamu hiyo, kampuni ya Wasafi Media ya kwake Diamond Platnumz iliweza kumpatia Barnaba Classic tuzo ya heshima kwenye usiku wa kuamkia leo katika Uzinduzi ambapo tuzo hiyo imelenga kusheherekea na kutambumbua mchango wa Barnaba Classix katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.

Ikumbukwe kuwa albamu hiyo ya "Love Sounds Different" kutoka ni ya 3 kutoka kwa Barnaba, albamu nyingine kutoka kwa msanii huyo ni pamoja na Gold ambayo iliingia sokoni mwaka 2018 pamoja na "Refresh Mind" iliyoachiwa mwaka 2020 na kuweza kupokelewa vyema na mashabiki.

Leave your comment

Top stories

More News