Cheed Aachia Tracklist Ya Ep Yake Ya "Endless Love"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Msanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide Cheed kwa mara nyingine ametetemesha kiwanda cha muziki Tanzania baada ya kuachia tracklist ya EP yake ya kuitwa "Endless Love".

Cheed ameachia orodha hiyo ya nyimbo zilizopo kwenye EP hiyo na wasanii walioshirikishwa ikiwa imetimia siku chache tangu atangaze kuachia EP hiyo ambayo inatarajiwa kuwa ni ya kwanza tangu aanze safari yake ya muziki miaka kadhaa nyuma.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Cheed alitangaza kuwa EP yake itasheheni ngoma 7 ambazo ni  Chombo, Roho Yangu, Kisu, Konkodi ambayo amemshirikisha Harmonize pamoja na Umenikatili ambayo amefanya First Lady wa Konde Gang Anjella.

Aidha Cheed alifichua kuwa EP yake imetayarishwa na mafundi mbalimbali wa muziki ikiwemo Terriyo Monster, Foxx Made It, Jacco Beats, The Mix Killer pamoja na Mocco Genius ambaye ana wasifu wa kufanya kazi na wasanii wengi wakubwa Tanzania ikiwemo Diamond Platnumz, Ali Kiba na wengineo wengi.

Kando na Cheed msanii mwingine ambaye ametangaza kuachia EP hivi karibuni ni pamoja na Nandy ambaye ametangaza kuachia EP yake ya kuitwa "Maturity" ambayo ameshirikisha wasanii mbalimbalk ikuwemo Dulla Makabila pamoja na Nviiri The Story Teller kutokea Kenya.

Leave your comment