Nyimbo Mpya: Harmonize 'Miss Bantu', Christian Bella 'Natamani' na Nyimbo Zingine Mpya Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kama unapenda muziki kutoka nchini Tanzania hasa muziki wa Bongo Fleva basi wiki hii huenda ilikuwa ni sukari sana kwa upande kwani wasanii wa Tanzania wengi wao wameweza kuachia ngoma kali mpya ambazo bila shaka zimeendelea kufanya soko la muziki kuwa jipya kabisa.

Kutoka kwa Harmonize, Ibraah, Tunda Man na wengineo, Zifuatazo ni ngoma tano mpya kutoka Tanzania wiki hii :

Miss Bantu - Harmonize Ft Spice

Harmonize hatimaye ameachia ngoma yake mpya ya kuitwa "Miss Bantu" ambayo amemshirikisha malkia wa Dancehall kutokea nchini Jamaica. Ngoma imetayarishwa na B Boy Beats na ndani yake anaeleza jinsi ambavyo ameshikwa kimapenzi na binti aliyekutana nae Nairobi.

https://www.youtube.com/watch?v=-NlD0zllsUc

Desh Desh (Video) - Lavalava

Kutokea WCB Wasafi Lavalava ameachia video ya Desh Desh ambapo Lavalava anaonekana akila raha na mpenzi wake katika mazingira tofauti tofauti huku akimuimbia mpenzibwake huyo. Video imeongozwa na Directir Hanscana kutoka Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=h0ArklhPZHI

Kizaazaa - Tunda Man Ft Ali Kiba.

Baada ya "Bad Man" kufanya vizuri hatimaye Tunda Man ameachia ngoma mpya kabisa ya kuitwa "Kizaazaa" ambayo amwmshirikisha Ali Kiba. Ngoma hii inaparikana kwenye EP mpya ya Tunda Man ya kuitwa "Tunda Man" na inatarajiwa kufanya vizuri.

https://www.youtube.com/watch?v=bxY9sMoflRY

Sitosema - Ibraah

Kutokea Konde Gang msanii Ibraah ameachia video yake ya kwanza kutoka kwenye album yake ya "The King Of  New School" ya kuitwa "Sitosema". Video imeongozwa na Director Ivan kutokea Tanzania na imetengenezwa na stori nzuri yenye ubunifu mkubwa huku ubora wa picha ukiwa umezingatiwa.

https://youtu.be/_C_FcTh6Z8M

Natamani - Christian Bella Ft Saraphina

Kwenye ngoma hii Saraphina anaonesha ni kwa jinsi gani anatamani kuolewa lakini Christian Bella ambaye anachukua nafasi ya mpenzi wake anasita huku akimsisitiza Saraphina kuwa na subira kuhusu jambo hilo la ndoa.

https://www.youtube.com/watch?v=02CFvYM2e_A

Leave your comment