Nyimbo Mpya: 'Melody' Diamond Platnumz na Nyimbo Zingine Zinazotamba Tanzania Wiki Hii
22 July 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo
Kama ulikuwa na kiu ya kufahamu ni ngoma gani kutoka nchini Tanzania ambazo zinafanya vizuri na kusikilizwa zaodi kwa wiki hii basi bila shaka makala hii ni kwa ajili yako, kwani imesheheni ngoma tano bora ambazo zinatazamwa na kusikilizwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.
Kuanzia kwa Diamond Platnumz, Mbosso, Zuchu, Harmonize na wenginezo zifuatazo ni ngoma tano kali zinazofanya vizuri nchini Tanzania kwa wiki hii.
Deka - Harmonize Ft Mabantu
Harmonize na Mabantu wameendelea kukimbiza kwenye kiwanda cha Bongo Fleva na ngoma yao ya "Deka" ambayo inazungumzua namna ambavyo pesa hutumika kushawishi wanawake kwenye mapenzi na kufikia sasa video ya ngoma hiyo imeshatazamwa mara Milioni 5.1 huko Youtube.
Melody - Diamond Platnumz Ft Jay Willz
Imechukua saa chache kwa Video ya "Melody" ya kwake Diamond Platnumz kushika nafasi za juu Youtube tangu kuachiwa kwake. Video hii ambayo imetengenezwa kwa ubunifu mkubwa na Director K kutokea nchini Nigeria imeshatazamwa zaidi ya mara laki nne na kuifanya kuwa video ya pili kutazamwa zaidi Tanzania kwa wiki hii.
Jaro - Zuchu
Video ya Jaro kutoka kwa Zuchu imeendelea kuweka rekodi ya aina yake kwenye mtandao wa YouTube kwani kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara laki saba ikiwa ni siku nne tangu kuachiwa kwake ikiwa ni mara pili kwa Zuchu kufanya kazi na Slowman Films kutokea nchini Nigeria.
Fire - Zuchu
Zuchu ameendelea kuwasha moto kiwanda cha Bongo Fleva na ngoma yake ya "Fire" ambayo pamoja na kwamba haina Video bado lakini imeendelea kufanya vizuri kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania kwani kufikia imeshasikilizwa mara Milioni 2.9 kwenye mtandao wa YouTube.
Moyo - Mbosso Ft Costa Titch & Phantom Steeze
Mbosso ameendelea kupeperusha bebdera ya Amapiano baada ya kuachia ngoma yake ya kuitwa "Moyo" ambayo ndani yake anaonesha ni kwa jinsi anataka kufanya starehe na video ya ngoma hii kufikia sasa imeshatazamwa takriban mara laki saba kwenye mtandao wa YouTube.
Leave your comment