Diamond Platinumz Aachia FOA Acoustic Akiisindikiza Na Video Mbili Za "Somebody" Na "Melody"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki mwenye kipaji cha aina yake kutokea nchini Tanzania Diamond Platnumz ameendelea kutoa dozi nzito ya burudani kwa mashabiki wake baada ya kuachia FOA EP Acoustic ambayo imesindikizwa na video mbili ambazo ni Somebody pamoja na Melody.

Kwenye FOA Acoustic Diamond Platnumz ameachia baadhi ya ngoma zilizopo kwenye toleo la kwanza la FOA lakini kwa sasa ametoa nyimbo hizo kwenye mtindo ambao ngoma hizo zinaweza zikasikiliza kwa uzuri zaidi huku ala za muziki kama gitaa na vinanda vikiwa vimepewa nafasi ya kusikika zaidi. Baadhi ya ngoma zilizopo kwenye FOA Acoustic ni pamoja na Melody, Mtasubiri, Sona, Loyal na Wonder.

Sambamba na toleo jipya la EP ya First Of All au FOA, Diamond Platnumz pia ameachia video mbili ambazo zinapatikana kwenye EP ya First Of All ambazo ni "Somebody" pamoja na "Melody" akiwa amemshirikisha Jay Willz kutokea Nigeria.

Kwenye Video ya Somebody ambayo imefanyika huko nchini Nigeria Diamond Platnumz anaonekana akiwa yuko kwenye kifungo cha mapenzi ambapo staa huyo anaonekana akiwa kwenye chumba amefungwa na mwanadada kisha baadae anaonekana akiwa amekamatwa kwenye utando wa Buibui huku akiwa anajaribu kujitoa ili aweze kumfuata mpenzi wake. Hii ni video iliyotengenezwa kwa Ubunifu mkubwa na pamoja na kuwa na wahusika wachache lakini haichoshi kuangalia.

Kwenye Video ya Melody ambayo ameifanya na Jay Willz Diamond Platnumz anavaa uhusika wa mwanaume ambaye amezama penzini na mwanamke. Video hii imeshirikisha wahusika wengi wa ziada (extras) ambao wanaonekana wakiwa wanahangaika kutafuta baridi kutokana na mazingira ya Joto waliyokuwepo.

Video zote hizo mbili "Somebody" na "Melody" zimeongozwa na Director K kutokea nchini Nigeria ambaye pia amehusika kutayarisha video ya Essence ya kwake Wizkid, video ambayo kwa mwaka 2021 ilikuwa ni video ya pili kutazamwa zaidi Youtube barani Afrika baada ya video ya Sukari ya kwake Zuchu.

Leave your comment