Nyimbo Mpya: Zuchu Aachia Video Ya Ngoma Yake 'Jaro'

[Picha: Instagram/Zuchu]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Zuhura Othman maarufu kama Zuchu kwa mara nyingine ameweza kuburudisha mashabiki zake nchini Tanzania baada ya kuachia video ya ngoma yake ya Jaro ambayo ilikuwa inasubiriwa sana na mashabiki.

Zuchu ambaye kwa sasa ndiye mwanamuziki anayeongoza kwa kuwa na wafuatiliaji wengi zaidi Youtube kwa upande wa wasanii wa kike, Kusini mwa Jangwa la Sahara ametoa video ya "Jaro" ikiwa imeshatimia takriban miezibsaba tangu aachie video yake ya mwisho ya kuitwa "Mwambieni" ambayo iliweza kutikisa Afrika Mashariki kwa ubunifu na stori yake ya kusisimua.

Video ya "Jaro" imetayarishwa kwa ubunifu mkubwa ambapo Zuchu anaonekana akiwa anacheza na kujiachia mbele ya mpenzi wake. Hii ni video ambayo imeendana na maudhui ya wimbo wenyewe ambao ni wa mapenzi huku kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa video ni wahusika wawili tu ambao wanaonekana ambaye ni Zuchu na mpenzi wake.

Video ya "Jaro" imetayarishwa na kampuni ya utayarishaji video kutokea Afrika Kusini ya kuitwa Slowman Films ambayo pia ilihusika kutayarisha video ya kwake Mbosso akiwa amemshirikisha Zuchu ya kuitwa "For Your Love" ambayo iliweza kupendwa na kuvutia mashabiki.

Ikumbukwe kuwa ngoma ya "Jaro" ni moja kati ya ngoma chache za Bongo Fleva ambazo ziliweza kuwa kubwa kabla ya kuachiwa. Mara ya kwanza kwa Zuchu kutumbuiza ngoma hii ilikuwa ni huko Lagos Nigeria kwenye tamasha la Youtube Africa Day Concert mwaka 2021.

https://www.youtube.com/watch?v=5kBlk8GsZlA

Leave your comment