Matukio 6 Yaliyoibuka Kwa Harusi Ya Nandy na Billnass

[Picha: Instagram/Cloudsfmtz]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Kama kuna jambo ambalo lilipamba wikiendi hii basi ni harusi ya mwanamuziki Nandy ambaye aliweza, kufunga pingu za maisha na rapa Billnass. Sherehe ya harusi kati ya wanamuziki hao wawili ambao kwa maracya kwanza walikutana kwenye tamasha la Fiesta, iliweza kuteka vichwa vya habari nchini Tanzania.

Yafuatayo ni mambo matano yaliyovuta umakini wa wengi kwenye harusi ya Nandy na Billnass.

Machozi ya Furaha Ya Nandy

Wakati anavalishwa pete na Billnass wakiwa kanisani KKKT Mbezi Beach Tangi Bovu, Nandy alilia kwa furaha kitu ambacho kilivuta hisia za watu wengi ambao walihudhuria ibada hiyo ya ndoa na amambao walikuwa wanafuatilia tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.

https://www.youtube.com/watch?v=MirQ4xlluQk

Msafara Wa Aina Yake

Barabara ziliweza kufurika kwa magari hasa wakati Nandy na Billnass wanatoka Kanisani ambapo barabara ya Mbezi Beach Tangi Bovu iliweza kujaa magari ambayo yalisheheni maharusi, wasaidizi wao, waandishi wa habari, wapambe, ndugu, jamaa na marafiki kitu ambacho kilipelekea barabara ya Bagamoyo Road kuwa busy sana kwa siku hiyo.

https://www.youtube.com/watch?v=VS6JYD0-h0o

Shabiki aliyevaa kama Diamond Platnumz

Wakati ibada ya Ndoa ikiendee,  shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Tumaini aliteka hisia za watu wengi baada ya kuvaa mavazi ambayo yalitengenezwa  mifuko ya "Shangazi Kaja", vazi ambalo linafanana na lile alilovaa Diamond Platnumz kwenye video ya "Oka".

https://www.youtube.com/watch?v=2oJ9uvXUPLY

Alikiba kuwaimbisha Maharusi "Utu"

Katika reception ya Harusi hiyo mmoja wa waalikwa Alikiba alipata nafasi ya kuwaimbia maharusi wimbo wake maarufu "Utu" na hata Bi. Harusu Nandy alimuimbia Billnass wimbo huo.

https://www.youtube.com/watch?v=HAI4gvKXHvg

Tambo za Steve Nyerere Na Mwijaku

Muigizaji Steve Nyerere pia aliweza, kupamba harusi ya Nandy Na Billnass kutokana na hari na hamasa aliyoitoa ambapo kabla ya kuingia ukumbi wa Mlimani City Steve Nyerere akishirikiana na Mwijaku walitanabaisha kuwa harusi ya Nandy na Billnass iligharimu Bilioni 5 kwa ujumla  huku akisema kuwa harusi hiyo ndiyo harusi kubwa ambayo ilishawahi kutokea Afrika Mashariki na Kati.

https://www.youtube.com/watch?v=yqeCwxZroLs

Tamko la Zuchu 

Malkia wa WCB Zuchu nae hakupitwa na harusi ya Nandy na Billnass kwani kupitia akaunti yake ya Instagram aliweza kuwapa  hongera za dhati Nandy na Billnass.

https://www.youtube.com/watch?v=kZXzWwlOzG0

Leave your comment

Top stories

More News