Manchester United na Usajili Mpya Wiki Hii
18 July 2022
[Picha: goal.com]
Mwandishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Balaa lingine la Manchester United linaendelea. Hili limekuja katika moja ya maandalizi ya kukamilisha usajili wa wachezaji mbalimbali.
Sasa wiki hii United wanaelekea katika hitimisho la kumsaini beki kutokea Ajax, Lisandro Martinez.
United wametangaza kuwa wako katika hatua za mwisho mwisho za kumsajili mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Argentina, Akitokea Ajax ya huko Netherlands.
Lisandro alisajiliwa na Ajax mwaka 2019 Akitokea Defensa y Justicia ya huko kwao Argentina.
Usajili huo wa United utakamilika Mara baada tu ya vipimo vya kimatibabu kukamilika. Manchester United wako tayari kutoa kibunda Cha Paundi milioni 57 ili waweze kumnyaka mchezaji huyo katika moja ya hatua za kuboresha safu yao ya ulinzi.
Kwa upande wa mkataba beki huyo anatarajiwa kusaini mkataba utakaodumu kwa takribani miaka 5 akiwa anakipiga huko Old Trafford.
Akiwa na umri wa miaka 24, Lisandro anatarajiwa kuongeza nguvu kwa mabeki wa United kama vile Aaron Wan-bissaka, Victor Lindelof, Harry Maguire ambaye yeye anayezungumziwa kwa kuwakera mashabiki wengi wa United akiwa uwanjani.
Katika msimu wa mwaka 2021/22 Lisandro alichukua tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka katika kikosi hicho Cha Ajax.
Mpaka Sasa mashetani hao wekundu baada ya kukamilisha usajili huo Basi utakuwa usajili wao wa tatu. Hili limekuja Mara baada ya kumsajili beki Tyrell Malacia na Christian Ericksen kwa msimu huu.
Leave your comment