Zinchenko Kuihama City Na Kukimbilia Arsenal

[Picha: express.co.uk]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kuelekea mbio za maandalizi ya ligi kuu ya Uingereza, Arsenal tayari wanaendeleza  harakati za kuimarisha kikosi Chao kwa msimu wa mwaka 2022/23.

Oleksandr Zinchenko Huenda akaondoka huko Ethihad Stadium na kwenda kujiunga na moja kati ya mahasimu wa Manchester City, Arsenal.

Hilo limekuja baada ya Arsenal kuikosa saini ya Raphina winga  aliyejiunga na Barcelona baada ya kutokea Leeds United ya huko huko EPL na kuikataa dili ya Arsenal.

Mchezaji huyo raia wa Ukraine mwenye miaka 25, tayari hatua za maandalizi ya kujiunga na Arsenal yameanza huku kukiwa hakuna dalili za kusuasua katika uhamisho huo.

Mikel Arteta tayari Yuko tayari kutoa kitita Cha Paundi milioni 35 kwa City Kama moja ya hatua za kumpata Zinchenko na kuimarisha kikosi Cha Arsenal.

Pep Guardiola inasemekana pia Yuko katika harakati za kutafuta

Beki mpya wa Kati na kutosheka na uwajibikaji wa Zinchenko katika kikosi Cha City baada ya msimu uliopita kutamatika.

Ijapokuwa hakuna upinzani mkubwa juu ya kuisaka saini ya Zinchenko lakini pia The Gunners wanakibarua Cha kuishinda nguvu ya The 'hammers' West Ham ambao nao pia wametupia jicho Lao kwa mchezaji huyo.

Mwaka 2016 Manchester City walimsaini mchezaji huyo Akitokea katika moja ya Timu za ligi kuu Russia Ufa. Usajili huo ulifanyika kwa jumla ya Paundi milioni 1.

Zinchenko ni moja Kati ya wachezaji wanaoweza kucheza nafasi mbalimbali katika uwanja wa kabumbu Kama vile beki wa Kati, kiungo wa Kati na pia winga.

Leave your comment