Rayvanny Aondoka WCB Rasmi

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Mac Voice Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Rayvanny hivi karibuni ametangaza rasmi kuondoka chini ya lebo ya WCB Wasafi ambayo inamiikiwa na mwanamuziki na staa maarufu nchini humo Diamond Platnumz.

Tangazo hili kutoka kwa Rayvanny linakuja miezi michache tangu kuwe na tetesi za msanii huyo kuondoka kwenye lebo hiyo kubwa Afrika Mashariki ambapo minong'ono ya kuondoka kwake ilipamba moto baada ya kutoa wasifu wa Wasafi kwenye Bio yake ya Instagram pamoja na kuwa kimya kwa muda bila kutoa ngoma mpya.

Rayvanny ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari za kuondoka kwake baada ya kuchapisha makala ya video fupi ambayo inaonesha safari yake ya kimuziki ndani ya WCB ambayo imedumu kwa takriban miaka 6 mpaka sasa ambapo amekuwa ni moja ya wasanii tishio Tanzania. Aidha kupitia makala hiyo Rayvanny alimshukuru Diamond Platnumz kwa kumuwezesha kuwa msanii mkubwa Tanzania

Kupitia WCB Rayvanny ameweza kuweka rekodi mbalimbali za kimuziki ikiwemo kuwa msanii wa kwanza Tanzania kushinda tuzo ya BET, kuwa msanii wa kwanza wa Tanzania kutajwa kwenye chati za Billboard Latin za huko Amerika ya Kusini pamoja na kuweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kutumbuiza kwenye jukwaa la MTV EMA.

Kando na Rayvanny wasanii wengine ambao tayari walishajitoa kwenye lebo ya WCB ni pamoja na Rich Mavoko pamoja na Harmonize ambaye aliondoka mwaka 2019 huku mwaka jana akifichua kuwa kilichomtoa WCB ni mgongano wa kimaslahi na lebo ya WCB Wasafi.

Leave your comment