Barnaba Classic Atangaza Kuachia Albamu Mpya "Love Sounds Album"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki nguli kutokea nchini Tanzania Barnaba Classic ametangaza, kuachia albamu mpya kabisa ya kuitwa LSD yaani Love Sounds Different ambayo ametangaza kuiachia ndani ya mwezi huu wa saba.

Barnaba Classic alitangaza ujio wa albamu hiyo kupitia mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya hivi karibuni ambapo Barnaba Classic alitanabaisha kuwa albamu yake itaitwa Love Sounda Different na inatarajiwa kuachiwa tarehe 28 mwezi wa Saba katika Uzinduzi wa aina yake ambao utafanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City Dar Es Salaam.

Barnaba pia alitanabaisha kuwa albamu hiyo inaadhimisha miaka yake 18 tangu aanze muziki hivyo albamu hiyo  itasheheni ngoma 18 ambazo zote atashirikisha wasanii tofauti na anatarajia kugawa asilimia 18 ya mapato yote yatakayotokana na albamu hiyo kwa ajili ya kusaidia makundi maalum.

Hii inatarajiwa kuwa ni albamu ya tatu kutoka kwa Barnaba Classic kwani  albamu yake ya kwanza iliitwa Gold na ilitoka mwaka 2018 ikiwa na ngoma 26 na ya pili ni Refresh Mind ambayo iliingia sokoni mwaka 2020 na ilikuwa imesheheni ngoma 16 ambazo ziliweza kuweka historia kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Kando na Barnaba, wasanii wengine ambao wametangaza kuachia albamu mwaka huu ni pamoja na Rosa Ree, Diamond Platnumz, Marioo na wasanii wengine wengi.

Leave your comment

Top stories

More News