Cristiano Ronaldo Aipalia Kaa La Moto ManchesterUnited

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Manchester United imeendelea kuonja joto la jiwe katika majira haya ya joto katika dirisha la usajili. Hii imekuja baada ya timu hiyo kuondokewa  na wachezaji wake mbalimbali waliomaliza mikataba yao na timu hiyo kushindwa kufanya usajili mpya. Wachezaji hao ni Kama vile Paul Pogba, Nemanja Matic, Dean Henderson pamoja na Juan Mata na wengine

Cristiano Ronaldo mshambuliaji wa timu hiyo anasemekana kutaka kuondoka katika viunga vya Old Trafford. Hii imekuja baada ya timu hiyo kuanza mazoezi ya mechi za kabla ya msimu kuanza licha ya kutokufanya usajili wowote.

Mshindi huyo wa tuzo tano za Balon dior ameonesha kutokupendezwa na Hali ya timu hiyo ya kutokufanya usajili mpaka Sasa licha ya kupungukiwa na wachezaji wengi baada ya mikataba yao kuisha.

Tetesi za mitandaoni zinaeleza kuwa Ronaldo angependa kumaliza maisha yake ya soka akiwa ameshiriki mashindano makubwa Kama vile Champions League. Lakini United wameshindwa kuweza kutimiza malengo ya mreno huyo.

Ronaldo akiwa mwenye miaka 36, alihamia United kwa mkataba wa miaka 2 Akitokea Juventus. Ukiacha na umri wake Ronaldo ameweka kambani mabao 18 katika msimu huu huko United.

Frenkie de Jong, kiungo wa Barcelona ni moja ya wachezaji walioonesha nia ya kutotaka kujiunga na timu hiyo. Huku Christian Eriksen akiripotiwa kukubali kujiunga na mashetani hao wekundu.

Ukiacha na Cristiano Ronaldo, hata pia mashabiki wa soka wa timu hiyo wameonesha kutokupendezwa na maendeleo ya timu hiyo katika miaka ya hivi karibuni. Hii imedhihirishwa na maandamano waliyoyafanya mwezi wa 5 mwaka 2021 wakiishinikiza familia ya Glazer kujiondoa katika umiliki wa timu hiyo.

Chelsea, Bayern Munich pamoja na Ac Roma ni moja ya timu ya ambazo zimewekwa katika orodha ya kumsaka mshambuliaji huyo ambaye anaendelea kuzeeka na makali yake.

 

Leave your comment