Vita vya usajili: Juventus kumsaka Firmino, Usajili wa Neymar Chelsea Waingia Hatua Ya Mazungumzo

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Gurudumu la usajili limeendelea kusonga mbele huku baadhi ya timu zikiendelea kuvuja jasho katika kusaka saini za wachezaji mbalimbali.

Zituatazo ni tetesi mbalimbali za usajili barani Ulaya zilizoshika vichwa vya habari.

Juventus

Mabingwa wa FA Cup huko England Liverpool Huenda wakamuondosha Mshambuliaji wao Robert Firmino. Juventus katika namesekana kuwa na jicho la tamaa kwa mshambuliaji huyo wa Kibrazili.

Staika huyo mwenye miaka 29 ameweza kuwa Bora zaidi alioshirikiana na miamba ya kiafrika  Sadio Mane anayeelekea Bayern Munich pamoja na Mohamed Salah katika msimu uliopita.

Kwa Firmino kwenda Juve inaweza ikawa moja ya makubaliano ya ya timu hizo mbili.Na hii ni baada ya liverpool kumtaka kiungo Adrien Rabiot.

Manchester United

Bado vigongo wa Old Trafford wanaendeleza mbio zao za kumfukuzia Frankie de Jong. Kiungo huyo Barcelona Amekuwa chagua la kwanza la Ten Hag tangu awasili United.

Ijapo kuwa Barcelona na Manchester United tayari wamesha kubaliana lakini De Jong ameonesha kutokuwa na nia wa Mashetani hao wekundu.

United wako tayari kutoa dau la takribani Paundi Milioni 65-70 ili kuupata wino wa kiungo huyo.

Chelsea

The blues tayari wameshaanza mazungumzo ni Katika moja ya hatua za kumpata Neymar. Baada ya Paris Saint Germain kuonesha kutokua na Nia na mshambuliaji huyo mapema hivi karibuni.

Hili limetokea miezi 12 baada ya mshambuliaji huyo kuongeza mkataba wake na PSG.

Kitendo Cha Kylian Mbappe kuongeza mkataba na PSG kinaweza kuwa sababu ya timu hiyo kutaka kumtimua Neymar katika klabu hiyo.

Leave your comment