George Mpole Kinara Wa Mabao NBC Premier League

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kwa Mara ya kwanza katika historia ya soka la Tanzania Timu ya Geita Gold Fc imemtoa mfungaji Bora katika msimu huu wa 2021/22 katika Ligi kuu ya Tanzania bara.

George mpole mshambuliaji wa timu hiyo ya Geita ameibuka kinara wa magoli katika msimu huu wa ligi kuu NBC. Hili limejidhihirisha mapema Juni 29 baada ya ligi hiyo kukamilika kwa Geita Gold kutoa sare ya bao 1-1 . Sare hiyo imemfanya Mpole kuwa mshindi wa tuzo hiyo ya mfungaji Bora katika mechi walicheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga

 

Mshambuliaji huyo wa Geita alikua akifukuziana na mashambiliaji ya Young African Sports club, Fiston Kalala Mayele. Mayele amemaliza Ligi hiyo akiwa na mabao 16 kwa maana ya bao 1 nyuma ya George Mpole ambaye ameweka kambani jumla ya mabao 17.

[Picha: Instagram/UFM]

Kwa George Mpole haikuwa kazi rahisi kwa yeye kuwa mfungaji katika  msimu huu. Na hii ni kutokana na kuwa kwa timu Kama Geita ambayo imepanda daraja katika msimu huu imefanya kazi kubwa sana. Si tu kwa George Mpole kuwa mfungaji Bora Bali hata kumaliza nafasi ya nne kwa Geita Gold Fc katika Ligi kuu imekua gumzo.

Kwa miaka ya hivi karibuni Katika Ligi kuu ya Tanzania bara Mara nyingi wafungaji Bora huwa wanatokea katika timu ya Simba. Kama vile John Boko aliyechukua tuzo hiyo katika msimu wa mwaka Jana huku Medy Kagere akichukua tuzo hiyo katika msimu wa 2020/21.

Geita Gold Fc katika msimu huu wameonesha ubora wa Hali ya juu kwa kumaliza nafasi ya nne na pia kumaliza msimu wakiwa na alama 49 katika ligi kuu hiyo.

 

Leave your comment