Nyimbo Mpya: Stamina Aachia "Ukizaliwa" muendelezo wa ngoma ya "Future wife" Amshirikisha Banana Zorro

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo

Rapa kutokea nchini Tanzania Stamina hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya kabisa ya kuitwa "Ukizaliwa" ambayo ni muendelezo wa series yake ya kimuziki ambayo ameipa jina la Love Bite.

Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Stamina ambaye ni mojawapo ya wanamuziki mashuhuri wa Hip Hop nchini Tanzania alitangaza kuachia mradi wake wa kimuziki wa kuitwa Love Bite ambapo msanii huyo aliahidi kuachia ngoma kwa mtindo wa episodes au sehemu ambapo kila ngoma itakuwa ni muendelezo wa ngoma nyingine.

"Future Wife" ilikuwa ni wimbo wa kwanza kwenye Love Bite Series, ngoma ambayo ndani yake Stamina amevaa uhusika wa mwanaume kapera ambaye anamuimbia mke wake mtarajiwa huku akiwa anajiuliza  maswali mengi kuhusu hatma yake ya kuoa.

Siku ya leo, Stamina kwa mara nyingine ameachia Ukizaliwa ngoma ambayo ni muendelezo wa Future Wife.  Kwenye ngoma hii Stamina anampa mawaidha na nasaha mtoto wake ambaye bado hajazaliwa akimuhasa mtoto huyo kuwa na bidii na kuwa maadili mema huku akimshirikisha msanii Banana Zorro.

Kitu cha kuzingatia ni kuwa Stamina ameonesha ubunifu mkubwa sana kwenye  ngoma hizi mbili yaani "Future Wife" na "Ukizaliwa". Pamoja na kwamba ngoma hizi zipo kwenye project moja ya "Love Bite" lakini maudhui na stori nzima ya kila wimbo unajitegemea. Ukisikiliza ngoma hizi mbili ni ngumu sana kung'amua kuwa stori zake zinategemeana au kwamba "Ukizaliwa" ni muendelezo wa "Future Wife"

Pamoja na utofauti huo wa kimashahiri pia itoshe kusema kuwa mirindimo na midondoko ya ngoma hizi mbili pia inashabihiana na kuendana kwani baadhi ya vichocheo vya kimuziki vya  kwenye ngoma ya kwanza ya "Future Wife" pia vinasikika kwenye ngoma ya "Ukizaliwa"

Ngoma ya "Ukizaliwa" imetayarishwa na mtayarishaji wa muziki ansyechipukiwa wa kuitwa Sampamba.

https://www.youtube.com/watch?v=6VHBO5l4It4

Leave your comment