Chelsea, Newcastle Kuisaka Saini Ya Neymar

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Winga wa Timu ya Taifa ya Brazil na pia Timu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar Jr. (30) Huenda akaondoka katika viunga vya Les Parc des Princes katika usajili wa majira haya ya joto

Taarifa hizi zimezuka baada ya Rais wa Klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi kuonesha Hali ya kutotaka kuendelea na mchezaji huyo wakati wa mahojiano yake na Le Parisien.

Rais huyo wa PSG kwenye mahojiano hayo alipoulizwa kuhusu  Neymar alisema "tunategemea wachezaji wetu wafanye vizuri zaidi ya msimu uliopita". Na Neymar kwa msimu uliopita akifunga mabao 13 pekee na kutengeneza pasi 8 za usaidizi wa magoli katika michuano yote  akiwa na PSG kwa msimu uliopita.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Baadhi ya timu za ligi kuu Uingereza zimehusishwa na kutaka kumsajili mchezaji huyo. Ila Sasa suala na Pesa linaweza kuwa zito kidogo. PSG inasemekana kuhitaji dau kubwa zaidi ili waweze kuitoa huduma ya Neymar kwa timu nyingine.

Chelsea wametajwa kama moja ya timu ambazo zinawinda saini ya mchezaji huyo wa kibrazili. Pia timu Kuna uwezekano wa kutoa dau la Paundi Milioni 76.6 ili Neymar awasili EPL kukichapa na Chelsea.

Toddy Boehly mmiliki mpya wa Chelsea tayari ameshatoa kitita Cha Poundi Milioni 200 ili timu hiyo ya Chelsea iweze kufanya usajili baada ya sakata la timu kufungiwa ilipokuwa chini ya Mrusi Roman  Ibrahimovic.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na PSG mnamo mwaka 2017 akitokea Barcelona na mkataba wake akiwa PSG unaotarajiwa kukamilika mwaka 2027 baada ya kuongezewa muda.

Mbali na Chelsea, Manchester United pamoja na Newcastle ambao wao wamepata mmiliki mpya pia wanahusishwa na usajili wa mchezaji huyo wa Kibrazili endapo ataondoka katika viunga hivyo vya PSG.

Wakati akijiunga na PSG Neymar alisajiliwa kwa kitita cha Euro Milioni 222 na kuwa moja ya wachezaji ghali zaidi kusajiliwa na timu hiyo.

Mwaka 2017 wakati Neymar anasajiliwa na PSG, pia Kylian Mbappe mshambuliaji wa Kifaransa alisajiliwa na PSG akitokea Monaco. Cha ajabu PSG waliomba Tena huduma ya Mbappe na kuongeza mkataba wake mapema mwezi huu na Sasa wanataka kumuuza Neymar mchezaji waliomsajili kwa dau kubwa zaidi.

 

Leave your comment