Marioo Akosoa Tabia Ya Ubinafsi Kwa Baadhi Ya Wasanii Wa Tanzania.
27 June 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo
Mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Marioo hivi karibuni amejitokeza na kuzungumzia upepo wa muziki wa Bongo Fleva ambapo msanii huyo amesema kwa kwa nchini Tanzania wasanii wakubwa huwa ni wale na hawabadiliki.
Marioo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya "Dear Ex" amefunguka hivi karibuni kwa kusema kuwa kwa muda mrefu sasa kwenye muziki wa Tanzania orodha ya wasanii wakubwa imekuwa haibadiliki na kutolea mfano jinsi mataifa mengine kama Nigeria yanavyoweza kukuza vipaji vipya vya muziki kila siku.
"Kuna Kipindi kimefika, inabidi tukubali kuwa Sisi ndio wasanii wakubwa wa Muda huu na hivi vitu huwa vinaenda na muda hata kwa mataifa mengine yaliyoendelea" "Ukiangalia Wenzetu Nigeria, Wasanii wakubwa walikuwepo kina D Banj, 2 Face, Don Jazzy wakina P Square, Baadae kikaja kizazi cha Kina Davido, Wizkid au Burna Boy, lakini sasa hivi unaona wamekuja madogo wamoto sana na wamepewa Ukubwa kwamba wao ndio wakubwa kwa sasa - wapo kina Rema, Joeboy, Fireboy, - Omah Lay au Kizz Daniel" aliseme Mario.
Marioo pia alifunguka kuwa kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tabia ya wasanii kuoneana wivu wenyewe ambapo baadhi ya wasanii wamekuwa hawaungi mkono kazi za wasanii wengine pindi zinapofanya vizuri.
"Tanzania kumekua na Tabia ya wasanii kuwekeana Kinyongo kwa msanii mmojawapo anapotengeneza Hit Kubwa kuliko wasanii wengine" "Unakuta Ngoma yako ndio namba 1 kwa wakati huo. lakini badala ya wasanii wote kuishikilia mfike mbali, wao ndio wanakua namba 1 kuikandamiza na kuweka vikwazo ili ifeli hiyo ngoma"alizungumza Marioo
Leave your comment