Madrid watupia jicho lao kwa Son Heung Min

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya kukosa kuwasajili washambuliaji wawili hatari zaidi katika Soka ambao ni  Kylian Mbappe wa PSG aliyeongeza mkataba na timu hiyo pamoja na Eirling Haaland aliyeamua kukimbilia Manchester City, Sasa Real Madrid imesemekana kutupia jicho lake kwa mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs Son Heung Min (29)  katika dirisha hili la majira ya joto.

Real Madrid inasemekana kumtaka mshambuliaji huyo mwenye asili ya Korea Kusini katika msimu huu, mchezaji huyo akiwa ndiye kinara wa magoli kwa msimu uliopita katika Ligi kuu ya Uingereza akifungana na mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah kwa kuweka kambani jumla ya mabao 23 na kushinda kiatu Cha dhahabu kwa msimu ulioisha wa 2021/22.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Suala lenye ukakasi linaweza kuja katika kumhamisha mashambuliaji huyo ni Je Antonio Conte Yuko tayari kuachana kinara huyo wa magoli ajiungea na miamba hiyo ya La Liga?, na huku katika msimu uliopita wa majira ya joto Son aliongeza mkataba utakaoisha mwaka 2025 huko Tottenham.

Lakini mpaka Sasa taarifa hizi hazijaweka wazi ni dau la kiasi gani Los Blancos wako tayari kulitoa ili Mkorea huyo aweze kujiunga na timu hiyo ya Jijini Madrid kwa msimu unaotarajiwa kuanza hivi karibuni lakini kwa tetesi tu Madrid wameweka kitita Cha Paundi Milioni 67.5 ili kumpata mchezaji huyo katika msimu huu wa 2022/23.

Winga huyo wa kushoto katika mechi zake 35 alizozicheza na Tottenham Hotspurs kwa msimu huu ni magoli 23 ametia kambani na kutengeneza pasi 9 za usaidizi wa magoli ambazo ndizo zimeifanya Tottenham Hotspurs kushiriki UEFA Champions League kwa msimu wa mwaka 2022/23 na kwa hili inaweza kuwa ngumu Sana kwa Conte kumuachia kirahisi Son ajiunge na Carlo Ancelotti.

Leave your comment