PSG Yakana Kuzungumza Na Zidane

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kitendo Cha Mauricio Pochettino kuondoka Paris Saint Germain mapema mwaka huu baada ya kuchukua ubingwa wa Ligue 1, mijadala mingi imezuka kwa mashabiki wa soka ambao wanahisi kuwa viatu vya kocha huyo wa Kiajentina vitavaliwa na mfaransa Zinedine Zidane katika kuinoa klabu huyo ya hukuhuko Ufaransa.

Tetesi hizo zimevuma kutokana na hali ya kuwa mpaka Sasa Zidane tangu amalizane na Real Madrid ya Hispania hajawahi kuifundisha timu nyingine yoyote na kutokana na utaalamu wake Kama kocha na kwa ukubwa la klabu ya soka kama PSG ndio uvumi huo wa yeye kwenda kuifundisha PSG ukasambaa.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Cha ajabu Rais wa Klabu hiyo ya PSG Nasser Al-Khelaifi wakati na mahojiano yake na chombo Cha habari Cha Le Parisien amekana klabu hiyo kuingia makubaliano yoyote na Zinedine kwa kusema, " Nitakwambia kitu kimoja, hatukuwahi kuongea nae moja kwa moja au kwa njia nyingine. Vilabu vingi vya soka vinaonesha Nia ya kumtaka hata pia timu za Taifa lakini hatujawai kuliongelea hili suala na yeye, Sisi tumemchagua kocha ambaye ni Bora Sana kwa kile tunachokihitaji kukiweka katika nafasi " Al-Khelaifi aliongezea.

Lakini mpaka Sasa PSG bado hawajamuweka wazi kocha huyo wanayetaka kumtumia katika mikakati ya klabu yao hiyo ya huko nchini Ufaransa, lakini moja ya malengo yao inaweza kuwa ni kuchukua ubingwa wa Ulaya kwa msimu ujao baada ya Real Madrid kuwatoa katika hatua ya Robo fainali kwa utofauti wa magoli 3-2 katika msimu uliopita licha ya PSG kuonesha kiwango kizuri zaidi katika michezo yote miwili waliyocheza na Madrid.

Ikiwa PSG imesajili wachezaji wengi waliobora zaidi katika uso wa dunia katika misimu Kama miwili ya nyuma na hii inaweza kuwa sababu ya timu hiyo kuwa Na uchu zaidi wa makombe makubwa ya nje na kwao kwa Sasa kinachohitajika ni kocha ambaye Yuko tayari kuinoa timu hiyo na kufikia malengo makubwa zaidi licha ya kuwa kwa Sasa wao ndio mabingwa wa Ligue 1 huko Ufaransa.

Leave your comment