Nyimbo Mpya: Mbosso 'Moyo', K2Ga 'Rangi Rangi' na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii
20 June 2022
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma Zake Nandy Bila Malipo Kwenye Mdundo
Ni wiki nyingine ambayo wasanii kutoka Tanzania wameendelea kujenga kiwanda cha muziki Tanzania kwa ngoma kali ambazo bila shaka zimeburudisha mashabiki na kuchangamsha tasnia ya Bongo Fleva.
Zifuatazo ni ngoma mpya kali kutoka Tanzani kwa wiki hii.
Moyo - Mbosso
Mbosso ameweza kuitendea haki ngoma ya Moyo ambayo amemshirikisha Costa Titch na Phantom Steeze kutokea Afrika Kusini. Kwenye Amapiano hii Mbosso anaonesha ni kwa namna gani moyo wake unahitaji raha na starehe baada ya kupitia dhoruba kwa muda mrefu.
Naacha Muziki - Dulla Makabila
Kambi ya Singeli wiki hii ilichangamshwa na Dulla Makabila ambaye kupitia ngoma hii alitangaza kuacha muziki iwapo mwanamuziki na CEO wa WCB Diamond Platnumz hatomsamehe baada ya wawili hao kukoseana. Hii ni ngoma ambayo Dulla anaomba radhi kwa Diamond Platnumz na timu nzima ya Wasafi.
Interview - Rapcha
Fundi wa kuhadithia hadithi kupitia ngoma zake, Rapcha, amerudi tena na "Interview" ngoma ambayo inapatikana kwenye EP yake ya kuitwa To The Top Volume 1. Kwenye mkwaju huu Rapcha anavaa viatu vya kijana anayewahi kwenda kwenye "Interview" ya kazi lakini haamini macho yake pindi anapofika kwenye kampuni anayotarajia kufanya Interview na kumkuta bosi wake
Rangi Rangi - K2ga
Sauti ya nzuri ya K2ga imeweza kupamba ngoma hii ambayo ndani yake K2ga anasifia namna ambavyo anapewa mapenzi moto moto na mpenzi wake. Hii ni ngoma ya kwanza ya K2ga ndani ya miezi 6 tangu aachie EP yake ya kuitwa Safari Novemba mwaka jana.
U&I - Abigail Chams
Baada ya kutia wino kwenye lebo ya Sony Music hatimaye Abigail Chams ameachia ngoma yake ya kwanza ndani ya lebo hiyo ya kuitwa "U&I". Hii ni ngoma ambayo Abigail anaonesha uwezo wa kisauti pamoja na ufundi wake kucheza na kufikia sasa imepokelewa vyema na mashabiki.
Leave your comment