Nyimbo Mpya: Diamond Platnumz 'Oka', 'Kioo' Anjella na Nyimbo Zingine Zinazovuma Bongo Wiki Hii

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Bila shaka mtandao wa Youtube umeendelea kuwa kipimo cha wimbo kufanya vizuri na wiki hii nchini Tanzania kama kawaida kuna ngoma ambazo zimeendelea kujiweka nafasi nzuri kwenye mtandao huo kutokana na mashabiki kupenda kazi hizo hivyo kuzitizama zaidi.

Zifuatazo ni ngoma tano ambazo zinavuma na kufanya vizuri kwa mtandao wa YouTube ndani ya wiki hii.

Oka - Diamond Platnumz Ft Mbosso.

Video ya "Oka" imeendelea kuwa namba moja Youtube kwa wiki ya pili mfululizo. Kufikia sasa video hiyo ambayo imetayarishwa na Hanscana na ambayo imeakisi maisha ya utamaduni wa Tanzania imeshatazamwa mara Milioni 4.7

https://www.youtube.com/watch?v=4G1tL5tQIsM

I Miss You - Rayvanny Ft Zuchu

Video ya "I Miss You" kutoka kwa Rayvanny imegharimu takriban  Milioni 40 za kitanzania ili kuikamilisha  na kutokana na bajeti yake ambayo imepelekea video hii kuwa bora sana mashabiki wengi wamevutiwa na kazi hii ambayo imeongozwa na Ivan na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 4.1 kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=EYfwcskpCis

Deka - Harmonize Ft Mabantu

Siku 7 tangu kuachiwa kwake  zimetosha kabisa kuwaaminisha watu kuwa "Deka" ni ngoma ambayo imependwa sana na mashabiki kutokana na mashairi yake mepesi na ubunifu mkubwa uliotumika, kufikia sasa ngoma hii imeshatazamwa mara laki tano themanini na tano kwenye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=RAsfgRc_paI

Badman - Tundaman & Harmonize

Tangu kuachiwa kwake, Bad man ya Tunda man na Harmonize imekuwa chaguo namba la wasikilizaji na kufikia sasa video ya ngoma hii imshatazamwa mara Milioni 2.4 huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=RS9PMaKJHQ4

Kioo - Anjella Ft Harmonize

Baada ya kupotea Youtube kwa siku kadhaa hatimaye video ya "Kioo" imerudi kwa kishindk huko Youtube na kufikia sasa imekusanya watazamaji Milioni 1.7 huko Youtube.

https://www.youtube.com/watch?v=gd5CMNZc8JM

Leave your comment