Abby Chams Wa Rockstar Afrika Afichua Jina La Ep yake

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Abby Chams Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanumziki kutokea nchini Tanzania Abby Chams hatimaye ameweka wazi jina la EP yake mpya ambayo anatarajia kuitambulisha sokoni siku chache zijazo.

Abby Chams ambaye kwa sasa yuko chini ya Uongozi wa Rockstar Africa lebo ambayo inaongozwa na Seven Mosha hivi karibuni akiwa kwenye mahojiano na Millard Ayo amesema kuwa anatarajia kuachia kazi mpya hivi ksribuni ambayo ni EP aliyoipa jina la Abby Gal na instarajiwa kuingia sokoni ndani ya mwezi Juni.

"Kuna EP inakuja inaitwa "Abi Gal" na its first single inatoka pia. Mimi I'm just excited kwa wote kuweza kusikia this new sound kwa sababu zamani mlikuwa mnamjua Abby lakini sasa hivi its Abi Girl na jina kabisa limebadilika. This symbolize now this is a new flavour a new sound" alizungumza Abby Chams.

Kuhusu sababu za kuamua kubadilisha jina lake la kimuziki kutoka Abby Chams mpaka Abi Gal, msanii huyo alidokeza kuwa uamuzi huo ni wa kwake na ameamua kubadilisha jina kwani kwa sasa mara baada ya kujiunga Rockstar na Sony Music anajiona kuwa mtu mpya.

"I fe like I've just gone through this change, kwamba nilivyoanza muziki and this journey I was just a little girl ambaye everyone just knew lakini sasa hivj i feel like I've just come up with a different sound hata mkisikia EP very different vibevery different sound. Kwa hiyo nilitataka kitu ambayo inge-symbolize that change and that shift" alizungumza Abby Chams.

Kando na Abby Chams wasanii wengine ambao wametangaza kuachia EP mwaka huu ni pamoja na Anjella kutoka Konde Music Worldwide huki wasanii wengine kama Diamond Platnumz, Ali Kiba, Harmonize, Rosa Ree na Zuchu wakiwa wametangaza kuachia albamu.

Leave your comment