Nyimbo Mpya: Navy Kenzo Waachia Ngoma Mpya "Manzese"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimayd kundi la muziki kutoka Tanzania la kuitwa Navy Kenzo hatimaye wamekata kiu ya burudani kwa mashabiki zao baada ya kuachia kibao kipya kabisa cha kuitwa "Manzese".

Ngoma ya "Manzese" inakuja takriban mwaka mmoja tangu Aika na Nahreel kuachia ngoma yao ya mwisho ya kuitwa "Nisogelee" ambayo iliingia sokoni Machi 5 mwaka 2021 huku video yake ambayo iliyatayarishwa na Director Ivan iliweza kufanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube.

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Kwa ufupi neno Manzese ni eneo maarufu sana jijini Dar Es Salaam ambako wengi wanapaita "uswahilini" na kwenye kibao hiki Aika na Nahreel wanatumia muktadha wa neno hili Manzese kusheherekea mapenzi yao. Huu ni wimbo ambao una vionjo vya dancehall na Bongo Fleva na katika ngoma hii Aika na Nahreel wanasifiana na kupongezana tangu walipokutana Manzese mpaka kufikia sasa wana watoto na familia.

Ngoma hii ni muendelezo wa wasanii kutoka Tanzania kupendelea kuzipa nyimbo zao majina ya maeneo mbalimbali, kwani kando na ngoma hii ngoma nyingine ambazo zimebeba maeneo maarufu ya Tanzania ni pamoja na "Mbagala" ya Diamond Platnumz, "Kimbiji" ya Bob Junior pamoja na "Dar Kugumu" ya Marioo, ngoma ambayo iliweza kufanya vizuri.

Ikumbukwe pia miezi michache iliyopita kundi hili la Navy Kenzo lilidokeza ujio wa albamu yao ya tatu ya kuitwa "Love & Dread" album ambayo pamoja na kwamba kundi hilo halijatangazwa  itatoka siku gani lakini mashabiki wengi wameshuku kuwa huenda albamu hiyo ikawa kwenye matayarisho.

https://www.youtube.com/watch?v=RW9_ih6-cSE

Leave your comment