'Young, Famous & African' Ya Diamond Platnumz Yatajwa Kuwania Tuzo Uingereza.

[Picha: premiumtimesng.com]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania baada ya tamthilia fupi aliyoshiriki mwezi Machi ya kuitwa "Young, African & Famous" kutajwa kuwania tuzo za filamu huko nchini Uingereza.

Filamu hiyo ambayo ilitengenezwa na kusambazwa na Netflix imetajwa kuwania kipengele cha "Kipindi Bora Cha Kimataifa" kwenye tuzo zinazoitwa "National Reality TV Awards" ambazo ni tuzo maalum kwa vipindi vya Televisheni ambavyo vinaonesha maisha ya watu wa kawaida bila kutumia hati au "script"

Kwenye kipengele hicho Young, Famous & African itachuana na vipindi vingine vya Televisheni vikubwa duniani kama vile "Hot To Handle", "Below Deck", "Selling Sunset" na nyinginezo nyingi huku kipindi hiko kikiwa ni kipindi pekee kutoka Afrika kimetajwa kuwania tuzo hizo kubwa nchini Uingereza kwa mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa Young Famous & African ni kipindi cha maisha halisi ambacho kiliandaliwa na kampuni ya Netflix na iliingia sokoni Machi 18 2022 na kuhusisha mastaa mbalimbali barani Afrika kama Diamond Platnumz, Zarina Hassan, Nadia Nakai, Khanyi Mbau na wengineo wengi.

Dirisha la kupiga kura kwa ajili ya tuzo hizo liko wazi mpaka kufikia Julai 20 na tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika Julai 28 mwaka huu huko Colchester jijini London Uingereza na kuhudhuriwa na mastaa wakubwa wa filamu duniani.

Leave your comment