Lacazette Aiacha Arsenal Na Kurejea Lyon

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya kudumu na klabu ya Arsenal kwa takribani miaka 5 huko Emirates stadium, Sasa Alexandre Lacazette ameamua kurejea Lyon ya Ufaransa baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu huko Premier League Uingereza.

Lacazette mwenye umri wa miaka 31 aliyesajiliwa kutoka klabu hiyo hiyo ya Lyon ameamua kuirejelea tena klabu hiyo iliyomkuza baada ya mwaka 2017 kuondoka katika klabu hiyo na kusajiliwa Arsenal kwa jumla ya Euro millioni 60 pamoja na bonus.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Tangu ajiunge na klabu hiyo ya Arsenal mshambuliaji huyo amecheza jumla ya mechi 206 na katika mechi hizo ameweza kufunga jumla ya mabao 71 na kutengeneza pasi za usaidizi wa magoli 30 akiwa na timu hiyo.

Akiwa na Arsenal "The Gunners" Lacazette ameweza kuchukua  komba la FA akiwa na timu hiyo akiisaidia timu hiyo kushiriki katika mashindano ya Europa league katika msimu ujao wa mwaka 2022/23 baada ya kupinduliwa na Tottenham Hotspurs katika kuisaka nafasi ya kushiriki UEFA Champions League.

Kwa kuongezea tu Alexandre ameutaka uongozi wa klabu ya Lyon kumsajili mchezaji Corentin Tolisso anayetokea klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu na kuwa mchezaji huru ili ajiunge na klabu hiyo ya Ufaransa katika kushiriki Ligue 1 sambamba akiwa na Alexandre Lacazette.

Leave your comment