Ubashiri Mechi ya Portugal Vs Czech Republic-UEFA

[Picha: CAFonline]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ni katika uwanja wa Estádio Josè Alvalade ambapo Ureno (Portugal) wanaenda kuwa wenyeji wa Jamuhuri ya Czech katika mzunguko wa 3 Ligi A, kundi 2 katika michuano ya mataifa ya Ulaya.

 Katika mchezo huo ambao timu zote mbili zinakutana bila ya kupoteza mchezo wowote katika kundi lao huku wakiwa na alama sawa kwa kila timu kuwa na alama 4, Ila Ureno akiongoza kundi hilo kwa tofauti ya magoli.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo

Katika mchezo huo ambao Ureno wanaingia wakiwa kifua mbele kwani katika michezo mitano mpaka Sasa ni mechi 3 wameibuka kidedea, mechi moja wametoa sare na mechi 1 wamepoteza.

Kwa upande wa Jamhuri ya Czech wao katika mechi zao tano wao wameweza kutoka na ushindi katika mechi 2 huku mechi 2 wakitoa sare na mechi moja wakashindwa kufua dafu na kufungwa.

Na kwa historia katika kuanzishwa kwa michuano hiyo Ureno ndiyo nchi ya kwanza kushinda mashindano hayo katika fainali waliyoicheza dhidi ya Netherlands katika msimu wa mwaka 2018/19 na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuweka historia.

kwa Sasa katika michuano hiyo bado ni mapema Sana kuweza kujua hatma ya katika msimu huu, hivyo Basi Odds za michezo ya kubashiri katika mechi hii ni double chance kwa Ureno wakipewa 1.12.

Leave your comment