Uchambuzi Mechi ya Tanzania Vs Algeria-AFCON

[Picha: CAFonline]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Katika kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), usiku wa Jumatano Tanzania iliwakaribisha Algeria katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mechi iliyochezwa majira ya jioni na matokeo kuisha kwa Tanzania kupata kichapo Cha bao 2-0 dhidi ya Algeria.

Katika mchezo huo Tanzania ameshindwa kuokota alama zozote ikiwa ni mechi yao ya pili katika kundi F baada ya kucheza na Niger mechi ambayo ikiisha kwa sare ya bao 1-1 na kuondoka kwa kugawama alama moja moja.

Katika mchezo huo wa Tanzania dhidi ya Algeria takwimu zinaonesha umiliki wa mpira kwa upande Tanzania ni 48.4% akizidiwa na Algeria ambao wao wakimiliki mpira kwa 51.6%, kwa upande wa kona Tanzania walipata Kona 3 huku Algeria wakifanikiwa kupata kona 1, Mashuti ya moja kwa moja Tanzania walikuwa nayo 2 na wao Algeria wakifanikiwa kupata mashuti 3, kadi za njano kwa Tanzania zilikuwa 2 huku Algeria wakipata Kadi 3 na katika mchezo huu Hakuna kadi nyekundu iliyotolewa kwa pande zote mbili.

Katika kundi F lenye nchi 4 Algeria ndiyo inaongoza kwa kuwa na alama 6 wakiwa wameshinda mechi zao zote 2 wakifuatiwa na Niger huku Tanzania na Uganda zikifuatan kwa timu zote mbili kuwa na alama moja moja katika kundi hilo.

Leave your comment