Nyimbo Mpya: Diamond ft Mbosso 'Oka', Kayumba 'Baishoo' na Ngoma Zingine Mpya Bongo Wiki Hii
6 June 2022
[Picha: Ghafla]
Mwandishi: Charles Maganga
Pakua Ngoma za Maua Sama Bila Malipo Kwenye Mdundo
Kama kuna wiki kwenye muziki wa Tanzania ambayo kiwanda cha Bongo Fleva kimepokea ngoma na nyimbo kali basi ni wiki hii. Mashabiki wengi wamefurahi na kutosheka kutokana na burudani wanayopata kutoka kwa wasanii wao. Zifuatazo ni ngoma tano kali ambazo zimeachiwa na wasanii wa Tanzania ndani ya wiki hii:
Oka - Diamond Platnumz ft Mbosso
Ushirikiano mzuri wa kisanaa kati ya Diamond Platnumz na Mbosso umeendelea kuonekana kupitia Oka; ngoma ambayo inapatikana kwenye EP ya Diamond Platnumz ya kuitwa First of All. Video ya ngoma hii imeongozwa na Hanscana na kufikia sasa imeshatazamwa mara laki tisa hamsini na tisa kwenye mtandao wa YouTube.
Baishoo - Kayumba
Ufundi wa Kayumba katika utunzi na uandishi wa Bongo Fleva umedhihirika kupitia 'Baishoo' ngoma ambayo Kayumba anaonesha na kukiri mapenzi aliyonayo kwa mwandani wake.
Sitaki Kujibu - Martha Mwaipaja
Martha Mwaipaja ametikisa muziki wa Injili wiki hii na wimbo wake wa 'Sitaki Kujibu'. Huu ni wimbo ambao Martha anasisitiza kukaa kimya na kutojibu chochote pamoja na kusemwa vibaya sana na watu wanaomzunguka huku akimuomba Mwenyezi Mungu amsaidie na kusimama kwa ajili yake.
Ronaldo - Weusi
Tasnia ya Hip-hop wiki hii imepokea bidhaa mpya kabisa ya kuitwa Ronaldo. Katika mkwaju huu, Weusi wanazungumzia hali ya mtaa, harakati za kimaisha na mambo ya kila siku kwa kutumia muktadha wa mpira wa miguu huku kiitikio cha wimbo huo kikimtaja mcheza soka wa Manchester United Cristiano Ronaldo.
Sishirikishi Mtu - Maarifa
Maarifa kutoka Manzese Music ameachia ngoma mpya wiki hii ya kuitwa 'Maarifa. Kwenye ngoma hio, Maarifa amechana na kurap kwa ustadi mkubwa kiasi cha kumkosha mwanamuziki Harmonize kutoka Konde Music Worldwide.
Leave your comment