Uchambuzi Mechi ya Simba Vs Yanga-ASFC

[Picha: africansports.today]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ni nusu fainali za kombe la Shirikisho Azam zimekamilika mwishoni mwa wiki baada ya shughuli kuisha kwa Young African Sports club kumaliza mchezo huo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Simba Sports Clubs katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Feisal Salum, Fei toto ndiye aliyetia kambani bao Hilo katika dakika ya 25 ya kipindi Cha kwanza na kuwaacha midomo wazi mabeki wa Simba kwa kutikisa nyavu za Simba kwa shuti moja matata Sana lililokosa upinzani kwa kipa wao namba 2 Beno Kakolanya aliyelinda lango la Simba katika mechi zote za kombe la Shirikisho Azam huku Aishi Manula alipokuwa akiuguza vidole.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Katika mchezo huu Simba walionesha kuutawala mchezo kumzidi mtani wake wa jadi kwani 54% ya mpira ulimilikiwa na Simba huku 46% mpira ilikuwa kwa wapinzani wao Yanga, huku mashoti ya moja kwa moja kuelekezwa lango la Yanga,Simba walipiga shuti 1 huku yanga wao wakipiga mashuti 3, kwa upande wa Kona Simba walipata kona 7 na Yanga wao walipata Kona 4,kadi zilizotolewa katika mchezo huo ni 2 zote za njano, Simba wakipata Kadi 1 na Yanga kadi moja na kadi nyekundu hazikuwepi katika mchezo huo.

Katika fainali Yanga watakutana na coastal Union ya Tanga baada ya kumtoa Azam katika nusu fainali iliyochezwa Jumapili kwa mikwaju ya penalti 5-6 mechi iliyochezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika jiji la Arusha Jumapili iliyopita.

Leave your comment