Ubashiri Wa Mechi Ya Liverpool Vs Real Madrid-Fainali UEFA

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Historia itaandikwa katika katika jiji la Paris pale ambapo Real Madrid mabingwa wa La liga watakapovaana na Liverpool kuwania ubingwa wa Ulaya Jumamosi hii katika uwanja wa Stade de France.

Ikiwa mpaka Sasa Los Blancos tayari wana mataji 13 ya ubingwa huo na Sasa wanasaka ubingwa wa 14 na Hakuna timu yoyote ya Ulaya ambayo inaikaribia Madrid kwa mataji hayo, kwa Majogoo wa Londoni wao ndio wanasaka taji la 7 la ubingwa wa Ulaya.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Katika suala la majeruhi kwa liverpool, Thiego Alcantara ndiye mchezaji anayewezakana kukosa mechi hii huku Mo Salah, Virgil Van Dijk wao wana nafasi kubwa ya kurejea uwanjani baada ya majeruhi waliyoyapata katika fainali za Carabao na pia Farbinho anauwezekano wa kurejea uwanjani, huku Divock Origi atakosa mchezo huo kutokana na matatizo ya misulu.

Na katika kikosi Cha Don Carlo Ancelotti vijana wake wako vizuri kiafya na anamawanda mapana zaidi ya kuchagua mchezaji yeyote na kufanya mabadiliko muda wowote.

Ni usiku wa rekodi kuwekwa kwa timu zote mbili na Jürgen Klopp kukosa ubingwa wa English Premier League ni Kama ameweka pembeni na kusahau kabisa Sasa nguvu kubwa iko UEFA na kupata taji hili kutamfanya akose taji moja la Ligi.

Huku Sheikh Karim Benzema kule Mohamed Salah, Vita ni vikali na Timu zote kupata magoli ndani ya dakika tisini Odds ni 1.62

Leave your comment