Uchambuzi Wa mechi ya Manchester City Vs Aston Villa-Epl Jumapili

[Picha: sportsstar.thehindu.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya mbio ndefu za msimu wa  Ligi kuu ya Uingereza kufikia tamati  Jumapili hii Sasa Basi mabingwa Manchester City wameweza kutetea ubingwa wao katika msimu huu Tena na kuwa ndio kombe pekee la ndani na njee kwa msimu huu walilopata.

Haikuwa kazi ndogo kwa City katika mchezo huo kwani katika kipindi Cha kwanza Cha mchezo huo Aston Villa waliongoza katika kipindi hicho Cha kwanza kupitia kwa beki wake  wa pembeni Matty Cash katika dakika ya 37 na katika dakika ya 69 ya kipindi Cha pili Aston pia waliongeza goli kupitia kwa kiungo mshambuliaji Philippe Coutinho waliomchukua kwa mkopo kutoka Barcelona na Sasa wameamua kumnunua kabisa.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Lakini Sasa City baada ya kuona Hali si swari na ni Kama vile tonge linapokonywa mdomoni baada ya vijana wa Steven Gerald kuwapelekea Moto ndipo Sub ya Ilkay Gundogan kuleta shamra shamra katika kipindi Cha pili kwa kufunga magoli mawili katika dakika ya 76 na 81 huku Rodri akifunga katika dakika ya 78 na huu ni ushindi wa City ndani ya dakika 5 tu.

Kwa ujumla Manchester City walimiliki 71% ya mpira na huku Aston Villa wao wakimiliki mpira kwa 29%, kwa upande wa Kona City walipata Kona 13 na Aston walipata Kona 1 tu, na mashuti ya moja kwa moja golini Manchester City walikuwa na mashuti 5 huku wapinzani wao wakiwa na mashuti 2 na kadi za njano zilikuwa 2 tu na zote zikitokea kwa Aston Villa.

Dakika 90 zikaisha na Manchester City wakabeba ubingwa wa pili mfululizo katika Ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa mwaka 2021-2022 chini ya Kocha wao Pep Guardiola.

Leave your comment