Ubashiri mechi ya Manchester City Vs Aston Villa-Jumapili hii

[Picha: birminghammail.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Hii ndiyo siku iliyosubiriwa katika Ligi kuu ya Uingereza ni katika kutaka kujua ni Nani haswa atakaye ondoka na ubingwa wa Ligi hiyo Jumapili hii.

Manchester City wakiwa katika viunga vyao vya Ethihad Stadium wanawakaribisha Aston Villa ili kukamilisha mzunguko wa mwisho wa Ligi hiyo.

Kuondoka na matokeo katika mchezo huu ndio lengo la msingi kwa City kwani Kama wataondoka na alama 3 Basi wao ndio watakua mabingwa wa Ligi hiyo kwa msimu uliopita huu wa 2021-2022 baada ya kukuchukua ubingwa huo kwa Liverpool.Hii ndiyo siku ya City na Liverpool kuombeana njaa baada ya kutofautiana alama moja tu kwani Liverpool wao wana alama 89 na City wakiwa na alama 90.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kikosi Cha vijana wa Steven Gerald Aston Villa, wao kupata matokea au kukosa katika mchezo huu hakuwezi kubadilisha Sana zaidi ya kupanda katika nafasi katika Ligi hiyo ama kushuka.

Sasa basi Aston Villa wanauhakika wa Mlinda mlango wao kurudi kikosini baada ya kuikosa mechi dhidi ya Burnley na mchezo huo kuisha kwa sare, majeruhi wengine ni walewale wakiwemo Kortney Hause, Ezri Konsa pamoja na Leon Bailey.

Katika upande wa kikosi Cha Pep Guardiola safu yake ya ulinzi inaonekana kuwa na mashaka baada ya wachezaji wake 2 katika safu hiyo kuonekana kuwa na majeraha na huenda wakashiriki katika mechi hiyo,wachezaji hao ni John Stone ambaye anasumbuliwa na misuli ya paja, Kyle Walker yeye alikuwa na shida katika kifundo Cha mguu huku Benjamin Mendy akiwa hayuko kikosini kutokana na makosa ya kinidhamu.

Manchester City watatumia jitihada zao zote kuhakikisha wanatoka na alama tatu ili kuchukua ubingwa huo hivyo Basi Odds za City kushinda mechi hii ni 1.16

Leave your comment