Uchambuzi Mechi ya Azam vs Simba iliyochezwa Jumatano

[Picha: bongo5.com]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Ni katika dabi ya Mzizima pale ambapo Azam Fc walipokutana na Simba Sc katika uwanja wa Azam Complex Chamazi ukiwa ni mzunguko wa 23 wa Ligi kuu ya NBC Premier League jumatano hii katika hatua ya kusaka alama 3 ili kuweza kusonga mbele kwa timu zote mbili.

Wana lambalamba Azam wakiwa nafasi ya 5 walitangulia kupata goli kupitia kwa Rodgers Kola alilolifunga katika dakika ya 38 huku wao Wekundu wa Msimbazi Simba wao wakiwa katika nafasi ya 2 alama 10 nyuma ya mtani wao wa jadi Yanga, walilazimika kukubali sare  katika mechi hiyo kwa kusawazisha dakika ya 45 ya mchezo kupitia mchezaji wake John Bocco katika dakika ya 45.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kipindi Cha kwanza ndicho kilichokuwa na bashasha zaidi Azam walicheza faulo 9 kwa 7 na mashoti ya moja kwa moja Azam katika kipindi Cha kwanza walipiga mashuti 4 na Simba wao walipiga mashuti 2.

Katika mechi hiyo kwa jumla ya umiliki wa mpira kwa Azam ulikua wa asilimia 54 huku wao simba wakimiliki mpira kwa asilimia 46 katika vipindi vyote  viwili, jumla ya Kona kwa Azam zilikuwa 3 na Simba walipata jumla ya Kona 4 katika mchezo huo.

Kama ilivyo ada uwepo wa kadi katika mchezo wowote wa soka ni kawaida hivyo Basi jumla ya kadi za njano kwa Azam zilikuwa 3 na Simba walipata Kadi moja tu ya njano na katika mchezo huu hakukuwa na kadi nyekundu.

Leave your comment