Uchambuzi wa Mechi ya Chelsea Vs Liverpool-Fainali za FA Cup

[Picha: Liverpool Instagram]

Mwandishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Fainali za Ubingwa wa FA Cup zimekamilika baada ya Liverpool kuchukua ubingwa huo mbele ya Chelsea kwa mikwaju ya Penalti.Hii ni baada ya dakika 90 kuisha bila ya kufungana na dakika za nyongeza pia kuisha na Sasa mikwaju hiyo ya penalti ndiyo iliyoamua mshindi katika uwanja wa Wembley Stadium.

Katika mchezo huo ambao katika suala la mashamulizi yalikua ni hatari kwa pande zote mbili zenye uchu wa matokeo umiliki wa mpira kwa Chelsea ulikua wa 45.5% huku Liverpool wao wakimiliki mpira kwa 54.5%.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kwa upande wa mashuti ya moja kwa moja Chelsea walipiga mashuti 4 huku Liverpool wao walipiga mashuti 6, katika Kona Chelsea walipata Kona 2 Ila Liverpool wao wakipata jumla ya Kona 11, Na offside Chelsea walikua na jumla ya Offside 7 Liver wakipata Offside 1 tu.

Katika suala la kadi Chelsea walipata Kadi za njano 3 na Liverpool wakipata kadi 1 ya njano na Hakuna kadi nyekundu kwa timu zote mbili.

Konstantinos Tsimikas ndiye mchezaji wa Liverpool aliyewapa ubingwa huo wa FA Cup baada ya Edwardo Mendy kushindwa kuipangua penalti yake na mpira kutikisa nyavu za Chelsea hatimaye Majogoo hao wa London Wakawika mbele ya Chelsea katika fainali hizo.

Mapema mwaka huu Ikumbukwe tu Katika fainali za Carabao Chelsea pamoja na Liverpool walikutana Tena na Liverpool wakaibuka washindi kwa kutikisa nyavu za Chelsea kwa jumla ya  mikwaju ya penalti 6-5 .

Leave your comment