Ubashiri mechi ya Wolveshampton Wanderers Vs Manchester City-Jumatano hii

[Picha: Betblog.com]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Katika kuelekea mwishoni kabisa mwa msimu wa Ligi kuu ya Uingereza Sasa Wolveshampton Wanderers wanaenda kukipiga dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi hiyo ya EPL Manchester City katika uwanja wa Molineux Stadium.

Wolves ambao kwa Sasa wako nafasi ya 8 katika Ligi wanasemekana kumrudisha uwanjani winga wao wa nyuma Daniel Podence aliyekua benchi kwa muda kutokana na majeraha ya kifundo Cha mguu.

Lakini pia watawakosa mabeki wake muhimu sana katika mechi hiyo ambao ni Max kilman pamoja na Nelson Semedo ambao wao wako nje kutokana na majeraha mpaka mwisho wa msimu huu kuisha.

Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com

Kwa upande wa vijana wa Pep Guardiola, Manchester City wao watawakosa wachezaji wake Kama vile Ruben Dias, John Walker pamoja na Kyle Stone huku Nathan Ake akiendelea kujikongoja na majeraha yake ya kifundo Cha mguu.

Kwa taarifa zilizotolewa na Meneja wa City amesema Fernandinho au Rodri wanauwezekano wa kuungana na Aymeric Laporte katika safu ya nyuma ya ulinzi.

Sasa basi wolves wao katika mechi zao 5 za hivi karibuni walizocheza wamepoteza mechi 3 wametoa sare mechi 1 na kufunga mechi 1 huku wao City katika mechi zao 5 za hivi karibuni wamepoteza mechi 1 na kushinda mechi 4 zilizobaki.

City katika mechi hii wanataka kujihakikishia ushindi kutoka kwa Wolve kutokana na kufukuziwa kwa Kasi Sana na Liverpool ambao kwa mpaka Sasa wana alama sawa katika msimamo wa ligi ya EPL wote wakiwa na alama 86.

Hii ni mechi itakayobeba shauku kwa mashabiki mbalimbali wa mpira hivyo Basi kwa watu wa kucheza michezo ya kubashiri Odds zilizotolewa kwa City kushinda mechi hii ni 1.22

Leave your comment