Tetesi Za Usajili Wa Mastaa Wa Soka Ulaya
11 May 2022
[Picha: Instagram]
Mwanadishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Huko Ulaya Sasa tetesi za mastaa wa soka kusajiliwa na kuhama timu zao zimezidi kusambaa katika mitandao mbalimbali, haswa katika Kipindi hiki ambacho ligi mbalimbali zikielekea ukingoni.
Wafuatao ni mastaa mbalimbali wa soka wanaosemekana wakahama timu zao baada ya msimu huu wa mwaka 2021-2022 kuisha.
Erling Haaland
Mshambuliaji kinda mwenye maajabu yake anasemekana kuwindwa na Manchester City katika dirisha kubwa la majira ya joto. Haaland mwenye miaka 21 amekua miongoni mwa wachezaji wadogo wanaosemekana kuweza kuja kuchukua nafasi ya kizazi Cha Messi na Ronaldo.
Manchester City inasemekana watatoa dau la Euro milioni 75 kwa Halland kutoka Borussia Dortmund na kwenda viwanja vya Etihad.
Lakini inasemekana mpaka Sasa tayari ameshaanza vipimo vya kimatibabu katika harakati za kujiunga na timu hiyo.
Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com
Pau Torres
Mhispania anayechezea Villarreal ya hukohuko Uhispania Sasa inasemekana anatakiwa na mashetani wekundu wa Old Traford kwa jumla ya Euro milioni 60 ili aweze kuhamia viwanja vya Manchester United.
Beki huyu mwenye umri wa miaka 25 anaweza kuleta marekebisho katika safu ya ulinzi ya United inayosemwa Sana kuwa ni mbovu.
Torres alitakiwa na United kwa muda Sasa lakini Varane ndio akachukua nafasi yake.
Romelu Lukaku
Baada ya kuwa na msimu usio na matunda kama ilivyotarajiwa Chelsea, Sasa Romelu Lukaku inasemekana anahitajika huko Italia kurudi tena kuchezea ligi hiyo ambayo alikipiga kwa misimu miwili.
Lukaku mwenye umri wa miaka 28 kwa Sasa Hana maajabu mengi Chelsea lakini inaoneshe Ac Milan kuna kitu wamekiona ndio maana inasemekana wako tayari kutoa takribani Euro milioni 100 ili waweze kumrudisha straika huyo huko Seria A.
Paul Pogba
Ni kiungo mwenye miaka 29 mpaka Sasa aliyenunuliwa kwa mara ya kwanza na Manchester United katika msimu wa mwaka 2011-2012 kutokea Le Harve lakini baada ya msimu huo kuisha aliondoka Kama mchezaji huru na kuhamia Juventus na ilipofika Tena mwaka 2016 United walimnunua kwa jumla ya Euro milioni 150 lakini kwa Sasa mwishoni mwa msimu huu anasemekana kuondoka Kama mchezaji huru na timu zinazomuwania ni pamoja na Juventus, Real Madrid pamoja na PSG na hii ni Kama hasara kwa United wanaomtoka Kama mchezaji huru baada ya kumnunua kwa mamilioni ya Euro.
Antonio Rudriger
Beki wa Kati wa Chelsea anasemekana kujiunga na Real Madrid ya Uhispania Kama mchezaji huru baada ya kukataa kuongeza mkataba na the Blues ambao ungeisha mwishoni wa msimu huu.
Mjerumani huyu anasemekana kusaini na the Blancos na pia atalipwa kiasi cha Euro milioni 9-10 kwa mwaka baada ya Kodi kukatwa.
Kuondoka kwa Rudriger huko Stanford bridge kunaweza kusababishwa na vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Uingereza kwa aliyekuwa mmiliki wa timu hiyo Roman Abramovich.
Bado tetesi ni nyingi na Kama ilivyoada kila mwisho wa msimu timu nyingi huangahika kutaka kuwapata wachezaji wanaodhaniwa kukidhi na kuleta maajabu kwa misimu inayofuata hivyo Basi yajayo yanaweza kuwa yanastaahisha zaidi.
Leave your comment