Uchambuzi wa Mechi ya Real Madrid Vs Manchester City-UCL
5 May 2022
[Picha: wwos.none.com.au]
Mwanadishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Usiku wa Jana wa Mabingwa wa Ulaya katika nusu fainali umekamilika katika mzunguko wake wa pili kwa Real Madrid kushinda na kukata tiketi ya kwenda fainali katika jiji la Paris baada ya kumfunga Manchester City kwa tofauti ya magoli 6-5.
Carlo Ancelotti kocha wa Madrid baada ya mechi ya Madrid na Manchester City kuisha aliongea na vyombo vya habari na kusema "Hakuna aliyedhani Madrid ingefika fainali 2021-2022 lakini tuko Hapo".Hii iliwanyima matumaini mashabiki wengi wa Madrid baada ya kuambulia magoli ya mapema katika mzunguko wao wa kwanza licha ya kujitahidi na kurudisha baadhi ya magoli.
Katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Real Madrid wa Santiago Bernabeu, City tayari walikuwa na mtaji wa bao moja mbele ya Los Blanco baada ya kuongoza katika mechi waliyocheza Etihad stadium katika mzunguko wa kwanza kwa mechi kuisha kwa jumla ya mabao 4-3.
Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com
Katika umiliki wa mpira Madrid walimiliki mpira kwa 46% huku wao City wakimiliki kwa 54%, na katika mashuti yaliyopigwa moja kwa moja katika lango la Madrid, City walikuwa na jumla ya mashuti 9 na wao Madrid wakiwa na mashuti 5 tu.
Kwa upande wa Kona vijana wa Carlo walipata Kona 3 huku City wakiwazidi kwa jumla ya Kona 9.
Katika suala la kadi zilikuweko kwani Madrid walikuwa na jumla ya kadi 4 za njano na Manchester City walipata Kadi 3 za njano na hakuna kadi nyekundu kwa timu zote mbili.
Katika dakika ya 73 ya mchezo huo Riyad Mahrez mfungaji wa Manchester City aliwainua washangiliaji wa timu hiyo baada ya kufunga goli na kuwapa wakati mgumu Sana Madrid kwa kuwa waliongeza tofauti ya magoli na kufika 3-5.
Ancelotti baada ya kuona Hali si swari katika dakika 68 ya mchezo alimtoa Tony Kroos na kumwingiza 'Super Sub' Rodrygo kinda wa miaka 21 wa Madrid na kuwapa raha Madrid kwani katika dakika ya 90 pamoja na dakika ya nyongeza 91 alisawazisha na kuwapa Madrid tumaini upya na Sasa wakiwa sawa katika magoli na kufanya waingie katika dakika za nyongeza.
Katika dakika za nyongeza 15 za kwanza Sheikh Karim Benzema alifanyiwa madhambi na kuwapa penalti Madrid iliyowasogeza mpaka fainali baada ya Benzema kutumia nafasi hiyo vizuri na kupata penalti hiyo.
Sasa basi katika fainali za mabingwa wa Ulaya zitakazochezwa Mei 28 katika uwanja wa Stade de France jijini Paris, Madrid watakutana na Liverpool waliowapa kichapo Villarreal, Ikumbukwe tu Katika fainali za UEFA 2018, timu hizi mbili zilikutana na Madrid ndio akachukua ubingwa huo wa UEFA.
Leave your comment