Mfahamu zaidi Kareem Mostafa Benzema

[Picha: Instagram]

Mwanadishi: Stellah Julius

Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani  ya Mdundo

Baada ya Karim Benzema kushinda hat trick dhidi ya Chelsea, mchezaji wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand kwenye mahojiano yake na kituo cha BT Sport alisema

"Karim Benzema ana miaka 34 na ndio namba 9 Bora duniani kwa sasa".

Karim Benzema alijiunga rasmi Real Madrid mwaka 2009 kutoka timu ya Lyon ya Ufaransa kwa Euro milioni 35 na kwa sasa anavaa uzi namba 9 katika viwanja vya Santiago Bernabeu huku kwenye timu yake ya taifa ya Ufaransa akicharaza uzi namba 19 .

Wengi wanamfahamu mchezaji huyu akiwa uwanjani tu lakini hivi hapa ni vitu vitano ambavyo wengi hawavifahamu kuhusu mchezaji huyu :

Safari yake ya mpira wa miguu

Benzema alianza kucheza mpira wa Mostafa Benzema ni mfaransa aliyezaliwa na wazazi wenye asili ya Algeria ambapo mama yake aliitwa Wahida Djebbara na baba yake aliitwa Hafid Benzema.Benzema alizaliwa Desemba 19, 1987 huko Lyon Ufaransa.

Alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 8 katika mji wa Bron ambapo ndipo alipozaliwa.

Karim aliaanza kuwavutia maafisa wa Lyon baada ya kufunga magoli mawili katika mechi iliyohusisha timu ya Bron Terroillon dhidi ya Lyon youth academy.

Hapo ndio maafisa wa Lyon walipotaka kumnunua kwenda kuichezea Lyon lakini Rais wa Bron  alikataa kumuachia Benzema kwenda Lyon .Shukran nyingi ziwaendee maafisa wa Lyon ambao walimaliza mazungumzo na wazazi wa Benzema na waliporuhusu tu, Karim Benzema alijiunga na timu hiyo.

Kujiunga Real Madrid

Mwaka 2009 Karim Benzema alisajiliwa kutoka Lyon kwenda Real  Madrid ingawa haikua rahisi kwake kwani msimu uliopita hakufanya vizuri sana hapo Lyon lakini baada ya kutafakari kwa muda kidogo alikata shauri na kujiunga na Real Madrid.

Kujiunga na kliniki ya kupunguza uzito

Benzema alihangaika Sana kuboresha kiwango chake kipindi akiwa anaanza kuchezea Real  Madrid.

Ili kuweza kuboresha kiwango chake Benzema aliwafuata magwiji wawili wa soka ambao ni Laurent Blanc pamoja na Zinedine Zidane ambao walimshauri staa huyo kuwa hana budi kupunguza uzito ili kuboresha kiwango uwezo chake uwanjani.

Katika kutekeleza ushauri huo Benzema aliamua  kujiunga na kliniki moja huko Italy na baada ya kurejea dimbani  msimu wa mwaka 2011-2012 mambo yalikuwa sukari kwa mfaransa huyo, kwani aliweza kupata mabao 32 katika msimu huo wa 2011/2012.

Benzema alifunga goli la dakika za mapema zaidi katika historia ya El classico

Benzema aliweka historia mpya kwenye historia ya La Liga baada ya kufunga goli  katika sekunde ya 22 kitu ambacho hakuna mchezaji wa Real Madrid au Barcelona aliyewahi kufanya.

Familia Ya Benzema

Karim Benzema ana ndugu 8 ambao watatu ni wavulana na watano ni wasichana na pia katika ndugu zake hao wawili wanasakata kabumbu ambao ni Gressy Benzema mwenye umri wa miaka 30 pamoja na Sabri ambaye alishawahi kuchezea timu ya vijana ya Bron. 

Tuhuma za kutaka kuvujisha video Chafu

Mwaka 2015 Benzema alishutumiwa  kutaka kisa Cha fedha zaidi ya maelfu ya Euro kutoka kwa Valbuena mchezaji mwenza wa timu ya Taifa Ufaransa au video na mpenzi wake ivujishwe katika mitandao ya kijamii.

Benzema inasemekana hakutaka kiasi hicho Cha fedha moja kwa moja Bali alitaka kitumwe kupitia kwa rafiki yake wa utotoni Karim Zenati.

Lakini kulingana na tuhuma hizo Benzema alikana kufanya kosa Hilo na baadae alikutwa na hatia na kupewa adhabu ya mwaka mmoja.

Shutuma hizi zilimfanya akataliwe kushiriki katika mashindano mbalimbali ya timu yake ya Taifa ya Ufaransa.

Mpaka Sasa Karim Benzema ni straika Bora sana katika timu ya Real Madrid huku akiongoza kwa mabao katika ligi ya La liga akiwa na magoli 25 katika mechi 34 mpaka Sasa.

Leave your comment