Uchambuzi Mechi ya Orlando Pirates Vs Simba walivyocheza Jumapili
26 April 2022
[Picha: Sportsbrief.com]
Mwanadishi: Stellah Julius
Pata na upakue Ubashiri wa Mechi mbalimbali ndani ya Mdundo
Ni katika marudiano ya robo fainali za michuano ya kombe la Shirikisho Afrika wakati Simba sports Clubs walipowasili katika viwanja vya Orlando Pirates Johannesburg katika hatua za kuwania kufudhu nusu fainali za kombe Hilo la shirikisho.
Katika mchezo huo umiliki wa mpira kwa Orlando Pirates ulikuwa wa 67% huku Simba wao wakimiliki mpira kwa 32% tu. mashoti katika lango la Simba,Orlando walipiga jumla ya mashuti 19,na Simba wao walipiga jumla ya mashuti 2 tu na yote yakiwa nje ya lango la Buccaneers hao.
Download FREE DJ Mixes on Mdundo.com
Katika mechi hiyo iliyojawa na mihemko ya aina ya kei, ilipofika dakika ya 58 ya mchezo huo Chriss Mugalu mchezaji wa Simba aliadhibiwa kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi Olisa Ndah.
Ilipotimia dakika 60 ya mchezo Orlando Pirates walitumia barabara udhaifu wa Simba wa kuwa na wachezaji pungufu uwanjani kwa kupata bao lao la kwanza kutoka kwa Kwame Peprah hivyo basi kusawazisha.
Wekundu hao wa Msimbazi,
Simba ambao wao tayari walikuwa na mtaji wa bao 1 baada ya kukutana na Orlando Pirates Jumapili iliyopita katika uwanja wa Mkapa wameaga mashindano hayo baada ya kulazimika kuingia katika mikwaju ya penalti dhidi ya pirates.
Katika mikwaju hiyo ya penalti Orlando wamefuzu robo fainali kwa kufunga penalti na 4,na Simba wao wakipata penalti 3 Kati ya 5 zilizopigwa.
Baada ya kuwaondoa Simba kwenye mashindano hayo, wanaenda kuvaana na Al Ahli Tripoli ya Misri.
Leave your comment